Nafasi Ya Matangazo

February 02, 2014

Meneja wa Huduma za Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi akikabidhi kitita cha shilingi milioni moja kwa mmoja kati ya washindi wa milioni moja Bw. Fadhili Musa Mbatu mkazi wa Temeke jijini Dar es salaam.Zaidi ya shilingi milioni 140 zimeshatolewa kwenye promosheni hiyo. Mwishoni mwa wiki.
 ********
Zaidi ya washindi 100 kote nchini wameshajishindia mamilioni ya pesa kupitia promosheni inayoendeshwa na kampuni ya mitandao ya simu za mkononi ya Airtel  inayofahamika kwa jina la Mimi ni Bingwa.
Kwa mujibu wa Meneja wa Huduma za kijamii wa kampuni hiyo, Hawa Bayumi alisema promosheni hiyo inaadhimia kuboresha maisha ya watanzania walio wengi kwa kurudisha sehemu ya pato la kampuni kwa wateja wake.
Wakiongea mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao baadhi ya washindi walisema kuwa pesa hizo zitawasaidia katika kutimiza malengo yao ya maisha na wengine wameainisha kuwa pesa hizo zitatumika kutatua  changamoto mbalimbali.
“Nilikuwa na mdogo wangu ambaye alikuwa akisumbuliwa na magonjwa mbalimbali, Pesa hizi nilizoshinda zitanisaidia katika kutatua  baadhi ya matatizo yaliyopo kwenye familia lakini bado haijatosha hivyo bado nitaendekea kushiriki mpaka nishinde hata ile zawadi kubwa ya shilingi Milioni 50,” alisema Bw. Mohamed  Mohamed mmoja wa washindi wa shilingi milioni moja wa wiki.
Aidha washindi hao wamesema wanaishukuru kampuni hiyo kwa kuonesha moyo wa kuwajali wateja wake na kutoa huduma zilizo bora kwa wateja hao.

Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo, Bw. Jackson Mmbando amezidi kutoa wito kwa wananchi kote nchini kuendelea kushiriki katika promosheni hiyo na kuendelea kujikusanyia pointi za ushindi kwa kuwa  airtel inakaribia kucheza droo kubwa ya shilingi milioni 50

 “ninaendelea kuwasisitiza wateja wetu wote endeleeni kushiriki kwa wingi katika promosheni hii ya Mimi ni Bingwa kwani ni kweli watu wanashinda na tayari Airtel imeshatoa zaidi ya shilingi milioni 200 kwa washindi mbalimbali” alisema Mmbando.

ili kujiunga na promosheni hiyo mteja anatakiwa kutuma neno Bingwa kwenda 15656 kisha kujibu maswali rahisi ili kujikusanyia pointi nyingi na kushinda mamilioni ya pesa au tiketi za kwenda Old Trafford..
Posted by MROKI On Sunday, February 02, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo