Nafasi Ya Matangazo

October 31, 2013

Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni ya Push Mobile Media Limited, Rugambo Rodney (katikati) akikabidhi funguo za magari kwa washindi wawili, Godfrey Michael (kulia), mkazi wa Keko Magulumbasi jijini Dar es Salaam na Crispine Ryakitimbo (kushoto), mwalimu wa Chuo Kikuu Cha St. John cha mkoani Dodoma baada ya kushinda magari aina ya Vitz katika promosheni ya fiesta iliyomalizika hivi karibuni.

Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya Push Mobile Media imekabidhi magari mawili aina ya Vitz kwa washindi wa promosheni ya fiesta iliyoendeshwa na kampuni  hiyo Tanzania nzima.
Waliokabidhiwa magari  hayo ni Godfrey Michael (25), mkazi wa Keko Magulumbasi jijini Dar es Salaam na Crispine Ryakitimbo (27), mwalimu wa Chuo Kikuu Cha St. John cha mkoani Dodoma.
Meneja Masoko na  Mauzo wa Push Media Mobile, Rugambo Rodney alisema kuwa wameshinda kwa ktuma neno Fiesta kwenda namba 15678 na kuingia katika droo. Rugambo alisema kuwa hatua ya kukabidhi magari hayo ni kukamilisha shindano hilo ambalo lilishirikisha watanzania katika tamasha la fiesta.
Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa, washindi hao waliishukuru kampuni ya Push Mobile Media kwa kuendesha shindano hilo na kujijengea imani kwa wateja wao kwani shindano hilo ni la ukweli.
Rugambo alisema kuwa mbali ya magari hayo mawili, awali walitoa magari mawili, moja kwa mkazi wa Kigoma na lingine kwa mkazi wa mkoa wa Mwanza.
Alisema kuwa pia waliweza kutoa pikipiki 12 zenye thamani ya sh milioni 1.6 kila moja na washindi 100 wa Sh 100,000  kwa kipindi chote tamasha la fiesta lilivyofanyika mikoani na kutoa zawadi zilizowagharimu sh milioni 80.
“Kukabidhi zawadi hizi ni kuhitimisha shindano la Fiesta ambalo tumeliendesha kwa kipindi cha miaka mitatu sasa na kutoa zawadi mbali mbali kwa jamii, tunaomba mtumie zawadi hizi kwa maendeleo na hasa kufanya biashara ya taksi,” alisema Rugambo.
Posted by MROKI On Thursday, October 31, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo