Nafasi Ya Matangazo

May 22, 2013

Mmoja wa wateja wa benki ya Blarclays ambaye pia ni Mwandishi wa Habari wa Magazeti ya Serikali, Regina Kumba akichagua moja ya majina katika droo ya bahati nasibu ya Beki hiyo ijulikanayo kama ‘Maisha Bomba na  Barclays Benki kupitia kampeni yake ya ya Sanduku la Dhahabu. Jumla ya washindi 13 walipatikana katika droo hiyo. Kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Barclays, Rahma Ngassa, Meneja wa Mawasiliano wa Barclays,Tunu Kavishe, Mwakilishi wa Michezo ya Kubahatisha, Humud Abdulhussein na Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Barclays  Samwel Mkuyu.

Meneja Masoko wa Barclays, Rahma Ngassa (kushoto) akizungusha pipa la bahati nasibu ya Beki hiyo ijulikanayo kama ‘Maisha Bomba na  Barclays Benki kupitia kampeni yake ya ya Sanduku la Dhahabu. Wengine pichani ni   Mwakilishi wa Michezo ya Kubahatisha, Humud Abdulhussein, Meneja wa Mawasiliano wa Barclays,Tunu Kavishe na Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Barclays  Samwel Mkuyu.
Meneja Masoko wa Barclays, Rahma Ngassa (kushoto) pamoja na viongozi wenzake wa Barclays Meneja wa Mawasiliano wa Barclays,Tunu Kavishe (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Barclays  Samwel Mkuyu wakiangalia pipa la bahati nasibu ya Beki hiyo ijulikanayo kama ‘Maisha Bomba na  Barclays Benki kupitia kampeni yake ya ya Sanduku la Dhahabu wakati wa kuchezesha droo za bahati nasibu hiyo leo. 
******     *******
Barclays Tanzania leo imefanya droo yake ya  kwanza ya kampeni  ya Maisha Bomba na Barclays Golden Briefcase kwa wateja wake muhimu wa sasa na wale wanaolengwa kwa baadaye.

Barclays leo imewapata washindi wake wa mwezi wa kwanza katika draw iliyofanyika katika ofisi zake hapa jijini dar es salaam.

Washindi hao 13 ni Erick Mahenge, Anna Erick Mahenge, Khalid,Taeko, Severin Rweba Celestin, Rashidi Saleh, Hemedi Ahmed, Saleh Koba Pili, Sheika Nasosr Salim, Hamid Khamis Othman, Arnold Rodrick Shirima, Jamal AA na Kaushal HJ, Jack Fales Kamata, Emmanuel Bernard Tungu, Pankaj Singh na Abdallah Rashid Khamis.

Akiongea na waandishi wa habari, Mkuu wa kitengo cha bidhaa Bwana.Samwel Mkuyu alisema, “Barclays ilizindua kampeni hii muhimu kwa wateja wao mwezi uliopita ambayo itawapa wateja wao muhimu fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali kila mwezi kwa muda wa miezi mitatu (3)”.

Bwana  Mkuyu aliongeza na kusema kuwa “ukiweka pesa yako benki na ukaweza kubakisha salio lililokusudiwa wewe ukiwa kama mteja wetu wa sasa na hata yule mpya ataweza kuingia kwenye droo ambapo wateja 13 watajinyakulia zawadi mbalimbali na mshindi wa jumla atajinyakulia zawadi ya tshs millioni kumi (10,000,000 TZS)” mwisho wa kampeni. Promosheni  hii ilizinduliwa rasmi tarehe11th April 2013 na itaendelea mpaka 30th June 2013.

Shindano hili liko wazi kwa wateja binafsi, wapya na wa zamani, ambao wanaweka fedha zao  na benki yetu hapa Tanzania. Wateja ambao watatakiwa kuingia katika promosheni hii ni wale tu wenye account ya hundi (Current Account) au amana (Savings), na wanatakiwa waongeze salio lao kwenye account kwa shillingi laki tano za kitanzania (500,000 tzs)au zaidi, na salio hili libakie kwenye account hadi mwisho wa mwezi bila kupungua, Kila ongezeko la shillingi Laki tano linampatia mteja ingizo la ziada katika katika droo ya mwezi husika..

Zawadi kubwa ya shilling million kumi za Kitanzania (shs. 10,000,000) itatolewa mwisho wa kampeni. Zawadi zote zitawekwa kwenye Barclays Golden Briefcase ambapo kila mshindi atatakiwa kuchagua mojawapo kisha kuifungua ili kujua alichojishindia.  Zawadi zinazoshindaniwa kila mwezi ni  iPads 2, vocha 8 za maduka makubwa ya bidhaa zenye thamani ya shillingi laki 2 kila mmoja (TZS200, 000), mashine za kuoshea nguo 2, na home theatre 1.
Posted by MROKI On Wednesday, May 22, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo