Nafasi Ya Matangazo

January 11, 2013


Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa,Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo kusini Mwa Afika SADC Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kulia) akiwa pamoja na Rais wa Madagascar Andry Rajoelina (kulia),Rais Wa Namibia Hifikepunye Pohamba (kushoto) na Rais wa Msumbiji  Armando Guebuza, wakati wa kikao cha Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama cha SADC, kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
 ******
NA  MAGRETH  KINABO – MAELEZO
WAKUU wa nchi na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuia ya Maendeleo ya  Kusini  Mwa Afrika(SADC  TROIKA)  wamekubaliana kusaidiana  na umoja wa Mataifa(UN) wa kupeleka  Majeshi ya  Ulinzi na Usalama(NIF)  katika upande wa  Mashariki mwa  Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo(DRC) .
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mtendaji wa Jumuia ya Maendeleo ya   Nchi za Kusini Mwa Afrika(SADC), Tomaz   Salomao wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa wakuu hao uliofanyika kwa muda wa siku mbili jijini Dares Salaam.
Mkutano huo ulimalizika leo  ambao ulikuwa unajadili hali ya siasa na usalama kwa nchi za DRC, Zimbambwe na Madagascar chini ya Mwenyekiti wake (SADC  TROIKA) Rais  wa Tanzania Jakaya Kikwete na kuhudhuriwa  na Rais wa  Namibia,  Hifikepunye Pohamba, Rais  wa Msumbiji , Armando Emilio  Guebuza, ambaye ni Mwenyekiti wa SADC na Rais wa Msumbiji , Jacob Zuma .
Akizungumzia kuhusu upande wa DRC   Salomao alisema “mkutano huo umetaka  misaada ya kibinadamu ipelekwe mapema iwezekanavyo katika upande wa Mashariki mwa DRC.
Salomao aliongeza kuwa wamepokea ahadi za nchi za Malawi, Namibia, Afrika Kusini na Tanzania za kuwa tayari kupeleka majeshi ya ulinzi na usalama katika upande huo , ambapo pia umezishauri  nchi nyingine ambazo hazijatoa ahadi hizo kufanya hivyo haraka iwezekanavyo.
Akijibu swali la mwandishi wa habari kuwa  kila nchi itachangia  wanajeshi wangapi na lini watakwenda Rais Kikwete  alisema suala hilo  bado liko kwenye mchakato.
Kwa upande wa Zimbabwe  Salomao alisema mkutano huo umependekeza  wadau  wa siasa katika nchi hiyo kuhakikisha  wanaharakisha  wanakamilisha utengenezaji wa Katiba mpya ili kuwezesha uchaguzi wa   amani, huru,  na haki .
Aliongeza kuwa  katika mgogoro wa kikatiba wa nchi ya Madagascar mkutano huo umepokea maelezo, kutoka kwa Rais  wa mpito wa nchi hiyo ,Andry Rajoelina kuhusu  mkakati wa kutatua suala hilo na kusisitiza utekelezaji wake.
Posted by MROKI On Friday, January 11, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo