Nafasi Ya Matangazo

January 11, 2013

 Sehemu ya Hoteli hoyo ya Nyota 5, inavyoonekana mbele yake kukiwa na 'Swimming Pool'.....
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Hoteli ya Kitalii ya Gold Zanzibar Beach House & Spa, Alexandro Azola (ushoto) wakati alipokuwa akitembelea kukagua maeneo na mazingira ya Hoteli ya hiyo, iliyopo Mkoa wa Kaskazini A, Unguja, wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo, mjini Unguja. Kulia ni Waziri wa Fedha, Zanzibar, Mhe. Omary Yusuph Mzee.
Makamu na ujumbe wake wakiondoka katika eneo hilo la Hoteli baada ya uzinduzi.
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Hoteli ya Kitalii ya Gold Zanzibar Beach House & Spa, iliyopo Mkoa wa Kaskazini A, Unguja, wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika leo, mjini Unguja. Kulia ni Waziri wa Fedha, Zanzibar, Mhe. Omary Yusuph Mzee, (wa pili kushoto) ni Mkurugenzi wa Hoteli hiyo, Alexandro Azola. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mhudumu wa mapokezi wa chumba cha mazoezi na masaji, Zuhura Saleh (kushoto) wakati alipokuwa akitembelea kukagua maeneo na mazingira ya Hoteli ya ya Kitalii ya Gold Zanzibar Beach House & Spa, iliyopo Mkoa wa Kaskazini A, Unguja, wakati wa hafla ya uzinduzi wa hoteli hiyo, uliofanyika leo, mjini Unguja. Kulia ni Waziri wa Fedha, Zanzibar, Mhe. Omary Yusuph Mzee.
 Moja ya sehemu ya Mandhari ya Hoteli hiyo........ 
 Mkurugenzi wa Hoteli hiyo akimuonyesha Makamu moja ya Chumba cha Hoteli hiyo......
Posted by MROKI On Friday, January 11, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo