Nafasi Ya Matangazo

September 03, 2012

Ni kama vile wanashindano kukatika lakini hapa ilikuwa show ya wacheza filamu Wema Sepetu (kul;ia) na Aunt Ezekiel wakiserebuka Ndombolo. katika jukwaa la Serengeti Fiesta 2012 jijini Mwanza.
JB akitoa hela katika waleti yake akitishia kuwatunza Wema na Aunt Ezekiel waliokuw wakicheza.
Mapacha watatu kutoka kushoto ni John Bukuku wa Full Shangwe Blog, Ahmad Michuzi wa Jiachie na Mzee mzima Mroki Mroki wa Father Kidevu Blog. Kikosi kazi hiki kulikuwa uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kukuletea haya yote.
Msanii wa Filamu Ray Kigosi akifanya vitu vyake kama Suoer Nyamwela.



Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti kutoka Clouds Media Group Bwa. Ruge Mutahaba akisoma namba ya mshindi aliyejishindia gari aina ya Vits ambazo zimekuwa zikitolewa  na kampuni ya Push Mobile katika mchakato mzima wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2012,Kati ni Meneja Masoko wa kampuni ya Push Mobile Bwa,Rugambo Rodney na shoto ni mmoja wa wakilishi wa bodi ya Taifa ya michezo ya kubahatisha Bwa.Bakari Maggid wakishuhutia tukio hilo usiku huu ndani ya uwanja wa CCM Kirumba.Mshindi wa gari hiyo aina ya Vitz alitajwa kuwa ni Bahati Joseph,mkazi wa jiji la Mwanza,mjasilia mali.


Baadhi ya mashabiki wakiwa wamejitokeza usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,linalofanyika kwenye uwanja wa ccm Kirumba.


Msanii wa bongofleva,Bob Junior a.k.a Shombe shombe akitumuiza na densa wake jukwaani


Pichani kulia ni msanii Recho kutoka THT akiwa sambamba na densa wake wakionesha umahiri wa kuimba jukwaani mauno kwa mbalii hivi.


Sehemu ya timu ya amsha amsha ya tamasha la serengeti fiesta 2012,kulia ni Dj Fetty,Bonge,Mully


Msanii wa kike anaekuja kwa kasi Recho akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu

Mwana dada Bahati akila pozi mbele ya gari lake alilolinyakua katika mahati nasibu y Gari ya Tamasha la Fiesta 2012 jijini Mwanza


Sehemu ya umati wa watu ukishangweka vilivyo usiku huu ndani ya uwanja wa ccm kirumba.


Msanii wa hip hop Roma Mkatoliki akiwa amepozi na mashabiki wake kabla ya kupanda jukwaani usiku huu.


Msanii Ney wa Mitego kama kawa akikamua kwa hisia mbele ya wakazi wa jiji la Mwanza (hawapo pichani) waliojitokeza kwa wingi ndani ya uwanja wa ccm kirumba.





Msanii Ommy Dimpoz pozi kwa pozi akitumbuiza jukwaani na kundi lake
Mzee wa Miduara katika anga ya muziki wa kizazi kipya,IT akiimba jukwaani.
Masharobaro ndio habari ya mujiniiiii....! Bob Junior na kundi lake wakitumbuiza kwenye jukwaa la Serengeti fiesta 2012 usiku huu kwenye uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza.
Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya aka Bongofleva,Prof Jay akishusha mistari yake kama kawa mbele ya umati wa watu (hawapo pichani),usiku huu ndani ya uwanja wa CCM Kirumba.
Mwanadada machachari kabisa awapo jukwaani,Mwasiti akiimba jukwaani usiku huu.
 Mkali wa sauti Barnaba akishambulia jukwaa
 Barnaba Boy akienda sawa na Steve Nyerere katika onesho hilo
 Roma Mkatoliki nae kama kawaida alitoa mistari yake ya maandiko katika Hip Hop.
Posted by MROKI On Monday, September 03, 2012 1 comment

1 comment:

  1. Picha bomba sana.....nimeupenda sana ujuzi wako mzee. Pata lightroom 3 kwa kuzichanganya vyema rangi...utaipenda.

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo