Nafasi Ya Matangazo

August 20, 2012

Pichani kati ni Mratibu wa shindano la Serengeti Fiesta Supa Nyota 2012,Antu Mandoza akiwataja vinara watatu kati ya 14 walioshindana vikali ndani ya ukumbi wa Sunciro usiku wa kumkia leo.Kutoka shoto ni Joh Maker (Morogoro),Ney Lee (Mbeya), sambamba na kijana mdogo lakini ni mwenye kipaji cha kufoka ile mbaya kutoka jijini Mwanza aitwaye Young Killa.Shindano hilo lilikusanya vijana mbalimbali wenye kipaji cha kuimba kutoka mikoa kadhaa ikiwemo Mbeya,Arusha,Morogoro,Tanga,Dar Es salaam,pamoja na jiji la Mwanza. Washiriki hao watatu watapa nafasi ya kuendelea kuonesha vipaji vyao kwenye matamasha yote ya Serengeti Fiesta 2012,ambayo inatarajia kuanza kurindiama Ijumaa ya wikii hii ndani ya jiji la Moshi-Chuo cha ushirika na jumipili litafanyika Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga
Burudani iliokuwa ikiendelea kutolewa na dani ya ukumbi wa Sunciro,washabiki walikuwa wakijimwa mwaya kwa staili hiyo huku wakiendelea kushuhudia shindano la Serengeti Fiesta Supa Nyota,lililokuwa na ushindani mkubwa kwa washiriki.
Mshiriki wa shindano la Serengeti Fiesta Supa Nyota 2012,Catrina kutoka jijini Arusha akionesha kipaji chake cha kuimba mbele ya umati mkubwa (haupo pichani) uliokuwepo kulishuhudia live tukio hilo ambalo pia lilikuwa likirushwa live na Clouds TV na Redio.
Majaji wa shindano hilo wakijadiliana jambo,kutoka kulia ni Othman Suka,Prodyuza wa Muziki Dunga,Dj Ibra pamoja na mtaalamu wa  mambo ya muziki kituo cha THT,Kardinal Gentlo.
Baada ya kuchuana vikali,washiriki 14,ukapitishwa mchujo mkali na kuwapata hawa washiriki sita pichani kama waonekanayo.Kutoka kulia ni Candy (DSM),Bridan Khan (Tanga),Ney Lee (Mbeya),Joh Maker (Morogoro) pamoja na You Killa kutoka Mwanza.
Ilikuwa ni full kushangweka ndani ya ukumbi wa Sunciro.
Mshiriki wa shindano la Serengeti Fiesta Supa Nyota 2012,Joh Maker kutoka mkoani Morogoro akionesha umahiri wa kipaji chake cha kufloo mbele ya sehemu ya mashabiki waliofika kulishuhudia live tukio hilo ambalo pia lilikuwa likirushwa moja kwa moja na Clouds TV na Redio.
Mshiriki wa shindano la Serengeti Fiesta Supa Nyota 2012,Candy kutoka jijini Dar akiimba na kucheza kwa umahri mkubwa mbele ya sehemu ya mashabiki (hawapo pichani) waliofika kulishuhudia live tukio hilo ambalo pia lilikuwa likirushwa moja kwa moja na Clouds TV na Redio.
Mshiriki wa shindano la Serengeti Fiesta Supa Nyota 2012,Ney Lee kutoka mkoani Mbeya akiimba na kucheza kwa umahri mkubwa mbele ya sehemu ya mashabiki (hawapo pichani) waliofika kulishuhudia live tukio hilo ambalo pia lilikuwa likirushwa moja kwa moja na Clouds TV na Redio.
Mmoja wa majaji,Dj Ibra akifafanua jambo kwa washiriki wa shindano la Serengeti Fiesta Supa Nyota 2012,shoto kwake ni mtayarishaji wa muziki aitwaye Dunga.
Mchakato wa majaji ulikuwa mgumu kuwapata vinara husika wa shindano hilo,kwani kila mmoja alijitahidi kuonesha uwezo na kipaji alichonacho.Kwa mujibu wa majaji wa shindano hilo walitoa vigezo husika kwa washiriki kuwa ni umiliki wa jukwaa na kujiamini,ubunifu wake wa kuimba,kuwepo mawasiliano kati yake na mashabi wanaotazama na pia kutoa maneno fasaha ili yasikike.
Washabiki mbalimbali walijitokeza kwa wingi kushuhudia shindano la Serengeti Fiesta Supa Nyota 2012,lililofanyika ndani ya ukumbi wa Sunciro jijini Dar,shindano hilo limefanyika likiwa na lengo ya kuinua vipaji vya kuimba kwa vijana kutoka sehemu mbalimbali,ambapo pia ilikuwa ni sehemu mojawapo ya mchakato wa kuanza kwa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Posted by MROKI On Monday, August 20, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo