Nafasi Ya Matangazo

June 18, 2012

Hawa watoto wanatia huruma sana. Wana umri wa mwaka na miezi saba, baba kaingia mitini kukwepa malezi mama yao, Arafa Ally (29) hana shughuli yoyote ya kumwingizia kipato.

Huyo mtoto wa katikati hawezi kukaa wala kusimama kwa sababu wenzake walimkalia tumboni kwa hiyo aliambiwa awe anampeleka hospitali afanyiwe mazoezi ili viungo vyake viwe imara aweze kusimama, lakini mama mwenyewe anaishi Kipera, Temeke hana uwezo wa nauli ya kila wiki na pia hana uwezo wa kusafiri na watoto wote watatu kwenye daladala kwenda Kiwalani kwenye kituo cha kumfanyia mazoezi.


Huyu mama alifika wiki iliyopita kwenye ofisi za Gazeti la Habari Leo kuomba aandikiwe taarifa zake angalau apate msaada wa mtaji wa kumwezesha kufanya biashara ndogondogo apate kipato cha kuwalea pamoja na kaka yao mwenye umri wa mia...ka 9.

.

Kwa jinsi alivyokuja ofisini, kwa mtu yeyote mwenye uchungu na watoto, angeguswa sana. Mtoto mmoja alibebwa na mwanaye mkubwa wa kiume mwenye umri wa miaka 9 halafu yeye akawa amembeba mwingine mgongoni na mwingine kambeba mkononi.


Fikiria sasa ni namna gani aliweza kugombea daladala!!!! Baada ya kufika katika ofisi za Gazeti la Habarileo, jamani watoto walikuwa na njaa kali. Mama yao alisema tangu asubuhi walikuwa hawajala kitu chochote kwa sababu alikosa unga wa kuwakorogea uji.

Walipopelekwa kantini, huwezi kuamini jinsi walivyokula wali. Huyu mama ANAOMBA ATAKAYEGUSWA, ANAWEZA KUMPATA KWA NAMBA 0655320169. 

Mzazi na Mlezi mwenye nguo, fedha, chakula au msaada mwingine wowote awasiliane kwa namba hizo awezeshwe kufikisha msaada kwa mama huyu aendelee kuwalea watoto hawa ambao ni MALAIKA
Posted by MROKI On Monday, June 18, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo