Nafasi Ya Matangazo

June 18, 2012

MSANII wa muziki wa kizazikipya nchini Nasib Adbdul ‘Diamond’ anatarajiwa kupamba shindano la kumsakaMiss dar Intercollege 2012 linalotarajiwa kufanyika Juni 22 kwenye ukumbi waMakumbusho ya Taifa , uliopo mkabala na chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Mratibu wa shindano hilo Dina Ismail alisema jana kwamba mbali na Diamond,onyesho hilo pia litapambwa na burudani kutoka bendi ya Skylight iliyopo chini ya mshirikiwa Tusker Project Fame mwaka juzi, Anneth Kushaba.

Alisema maandalizi yashindano hilo yanakwenda vema ambapo warembo 14 watakaosghiriki  wanaendelea na mazoezi katika hoteli ya  The Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dares Salaam

 “Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmojaya warembo kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema Dina.

Warembo watakaoshirikishindano hilo  wanatoka vyuo vya  Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) naTime,  Ustawi wa Jamii,  Usimamizi wa Fedha (IFM)  na Chuo Kikuu huria (OUT ambapo tajilinashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM, huku mshindi wa pili wa mwaka jana,Blessing Ngowi alitinga fainali za Miss Tanzania.

 Dina aliwataja warembo haokuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda  Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael,Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, SaadaSuleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.

 Shindano hilo limedhaminiwana kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s,Dodoma Wine, NdegeInsurance, Skylight Band,Lamada Hotel, Screen Masters,Makumbusho ya Taifa,Mustafa Hassanali, Shear Illusions, Lamada Hotel,Grand Villa Hotel, SportiKizaa zaa, Clouds Fm na blog za Michuzi, Mamapipiro, Bin Zubeiry,Mtaa kwa Mtaana Fullshangwe.
Posted by MROKI On Monday, June 18, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo