Nafasi Ya Matangazo

May 09, 2012

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliamua kupanda Pikipiki na kujitambulisha kama mmoja wa wadau wa bodaboda na kusema kuwa anatambua mchango wao katika sekta ya usafiri nchini haswa kwa watu wa kipato cha chini. Alitumia mwanya huo kuwaelezea umuhimu wa wao kujiunga na mfuko wa bima ya afya ambapo walionekana kuhamasika na kuahidi kujiunga na mfuko huo mapema iwezekanavyo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akihamasisha waendesha pikipiki katika Manispaa ya Sumbawanga kujiunga na mfuko wa bima ya afya leo katika viwanja vya shule ya sekondari Msakila. Alisema kuwa waendesha bodaboda wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ajali za barabarani jambo lililosukuma kupewa vizibao hivyo maalum vitakavyosaidia kuonekana kirahisi wawapo barabarani, aliwasihi kujiunga na mfuko huo kujihakikishia usalama wa afya zao pindi wapatapo matatizo ya ajali au maradhi ya kawaida.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi Wegson Frakson kiongozi wa kikundi cha waendesha pikipiki cha Soko Kuu Mandela vizibao maalum vya usalama barabarani kwa ajili ya waendesha bodaboda Mkoani Rukwa leo, vizibao hivyo vimetolewa na mfuko wa bima ya afya nchini NHIF kwa vikundi tofauti 15 vya waendesha pikipiki katika Manispaa ya Sumbawanga. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Ndugu Hamis Mdee.Vizibao hivyo vinaakisi mwanga utakaosaidia dereva wa bodaboda kuonekana kirahisi awapo barabarani hivyo huepusha uwezekano wa kupata ajali.
Posted by MROKI On Wednesday, May 09, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo