Nafasi Ya Matangazo

May 09, 2012

Rahwa Afeworki (22)- Eritrea
 
Warembo watakaoziwakilisha Nchi zao katika mashindano ya Miss East Africa mwaka huu wameanza kutangazwa.

Mrembo wa kwanza kupatikana ni Miss Rahwa Afework (22) kutoka Nchini Eritrea ambaye aliwashinda wenzake waliojitokeza kutaka kuiwakilisha Eritrea katika mashindano hayo.

Miss Rahwa Afework mwenye urefu wa 1.73m anasomea mambo ya Fashion design Nchini Eritrea.

Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitafanjika tarehe 07 mwezi September mwaka huu jijini Dar es salaam ambapo zitashirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius.

Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam
Posted by MROKI On Wednesday, May 09, 2012 2 comments

2 comments:

  1. AnonymousMay 09, 2012

    she so beautifu

    ReplyDelete
  2. MaProsooMay 10, 2012

    Kaka,

    Mbona umetutolea wa Eritrea tu?
    Si ungetutolea na wa RWANDA kabisa umalize mambo?

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo