Nafasi Ya Matangazo

January 05, 2012



TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI
TAHADHARI YA ONGEZEKO LA MVUA MAENEO YA KUSINI
MWA NCHI.

Msimu wa mvua unaendelea katika maeneo yanayopata mvua mara moja kwa
mwaka (mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Morogoro kusini,
Rukwa, Dodoma, Singida, Kigoma na Tabora.)

Katika kipindi cha siku tano kuanzia Januari 5 hadi Januari 10, 2012, mgandamizo mdogo wa hewa katika eneo la rasi ya Msumbiji unatarajiwa kuendelea kuimarika hivyo kusababisha ongezeko la mawingu katika maeneo ya kusini mwa nchi. 

Hali hii inatarajiwa kuimarisha makutano ya upepo wenye unyevunyevu katika maeneo hayo, hivyo kusababisha vipindi vya mvua kubwa katika maeneo ya Nyanda za juu kusini magharibi (mikoa ya Iringa, Mbeya na Rukwa), maeneo ya kusini (mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi), baadhi ya maeneo ya Kusini mwa mkoa wa Pwani na Kusini mwa mkoa wa Morogoro (Mahenge). 

Aidha  mvua za kawaida za masimu zinatarajiwa kuendelea kunyesha katika  maeneo ya kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida) na magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma na Tabora). 

Maeneo ya Pwani ya kaskazini ( mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani na visiwa
vya Unguja na Pemba), baadhi ya maeneo ya Nyanda za juu kaskazini mashariki
yanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua ambazo ziko  nje ya msimu.

Mvua hizi zinatarajiwa kuambatana na upepo mkali katika maeneo ya Bahari ya
Hindi, hivyo watumiaji wa Bahari wanashauriwa kuchukua tahadhari. 
Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya Hali ya
hewa na athari zake na itaendelea kutoa taarifa.

IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.
Posted by MROKI On Thursday, January 05, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo