Nafasi Ya Matangazo

January 05, 2012

Basi la abiria la kampuni ya Taqwa linalofanya safari zake kati ya Dar-Kigali nchini Rwanda limeanguka katika eneo la Mikese, Morogoro wakati likiwa njiani kuja jijini Dar na kujeruhi watu kadhaa waliokuwepo kwenye basi hilo.Chanzo cha ajali ni lori la mizigo lililokuwa limeegeshwa barabarani kutokana na ubovu, pia mwendokasi wa mabasi,kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo.wakati huo huo Basi la Morobesti limenusurika kuanguka japo liliacha njia kutokana na chanzo hicho hicho cha Lori lililoharikiba na kusimama barabarani.
lakini pia tunaweza jiuliza ni kwanini wamiliki wa Mabasi haya huamua kufuta majina yao au kufunika na magazeti pindi tu itokeapo ajali?
Msururu wa magari katika eneo la ajali.
Basi la kampuni ya Morobesti likiwa limeacha njia na kutoka nje ya Barabara kama linavyoonekana pichani hapa likifanyiwa mpango wa kuvutwa na Break Down inayoonekana hapa katika eneo la ajali.Picha na Mdau Rajab
Posted by MROKI On Thursday, January 05, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo