Nafasi Ya Matangazo

November 09, 2011

Meneja huduma na Bidhaa wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Bw. Elihuruma Ngowi akionyesha Tablet V9 moja ya zawadi ya zitakazotolewa kwa washindi wawili wa kwanza katika fainali za shindano la TIKISA litakalofanyika mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na Vodacom (kushoto) ni Meneja wa Power House Ndg. Octavian Francis.
Meneja wa Vodashop Mlimani City. Happiness Macha akitoa maelezo kwa washiriki wa shindano la TIKISA baada ya kuwapatia vipeperushi vyenye kuonyesha huduma mbalimbali zitolewazo na Vodashop ambazo ni pamoja na M-pesa, vifurushi vya internet na nyingine nyingi wakati walipotembelea kujionea na kujifunza huduma zinazotolewa katika Duka hilo.
Meneja huduma na Bidhaa wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Bw. Elihuruma Ngowi akiaonyesha zawadi mbalimbali za simu za mkononi kwa washiriki waliofanikiwa kuingia fainali za shindano la TIKISA ambao ni Helen Mangare, Hawa Mohamed, Hassan Said na Daniel Tobias wakati walipozuru Makao makuu ya Vodacom Mlimani City Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Vodacom Najenjwa Mbaga (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa washiriki wa fainali za TIKISA kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na kitengo hicho kwa wateja wake pindi walipopata fursa ya kutembelea Makao makuu ya Vodacom Tanzania (kulia kwake) ni Meneja wa huduma kwa wateja Bi. Edith Ezekiel.
Washiriki wa fainali za shindano la TIKISA wakipata maelekezo kutoka kwa Mtoa huduma kwa wateja wa Vodacom Bw. Nemes Kimati jinsi wanavyohudumia wateja wao pindi walipotembelea Ofisi za Vodacom Tanzania ikiwa ni safari yao kuelekea katika kilele cha shindano hilo mwishoni wa wiki.
Posted by MROKI On Wednesday, November 09, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo