Nafasi Ya Matangazo

November 09, 2011

Mkurugenzi wa Operesheni wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) Eugin Mingongoti akipokea tuzo ya Ushiriki Uliotukuka katika kutoa Huduma Bora za afya kwa Niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, kutoka kwa Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Gaudensia Kabaka wakati wa Maonesho ya Miaka 50 ya Uhuru yaliyoandaliwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inayoratibiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa NHIF wakifurahia kwa pamoja Tuzo hiyo kwenye banda la NHIF ambapo Mfuko wa taifa wa Bima ya Afya umepata kutokana na utoaji wa Huduma zaupimaji wa afya Bure kwa wananchi na wanachama wake. Katikati ni Mkurugenzi wa Operesheni wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) Eugin Mingongoti  na kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha Deusdedit Tutazaa na kulia ni Ofisa wa Idara ya Uanachama Neema Msanya.
Mmoja wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam Mohamed Juakali akipata huduma ya bure ya kupimwa kisukari kutoka kwa Dr. Eshe Juma. Upimwaji hufanyika burekatika banda la NHIF.
Posted by MROKI On Wednesday, November 09, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo