Nafasi Ya Matangazo

October 02, 2011

Airtel Tanzania yapunguza gharama za mawasiliano kupiga simu nchi za Afrika mashariki
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sam Ellangallor
  • Mtandao wa mawasiliano waendelea kutoa gharama nafuu za mawasiliano kwa nchi za afrika mashariki
  • Sasa kuongea na jirani zetu afrika mashariki kwa punguzo la hadi sh   2  na senti 50 tu kwa sekunde.
  • Gharama nafuu ya mawasiliano ni nyezo muhimu katika kusaidia kukuza uchumi wa nchi

Dar es Salaam, Tanzania 02 Octoba 2011 Airtel Tanzania imetangaza gharama mpya za kupiga simu Kenya na Uganda. Kupitia punguzo hilo wateja wa Airtel ndugu na jamaa zao sasa wataweza   kufanya biashara kwa urahisi hasa zile zinazohusisha kuvuka mipaka ya nchi yetu na kuhusisha nchi za  Kenya au Uganda kwa punguzo nafuu sana la Tsh 2 na senti 50 tu badala y sh 5 na senti 16

“Huu ni muendelezo wa kati ya dhamira endelevu tulizonazo Airtel kuwapa unafuu hasa wafanya biashara kuweza kufanikisha mahusiano yao kibiashara kati ya nchi moja hadi nyingine”

Akisisitizia Dhamira hiyo ya kupunguza mawasiliano simu za kwenda nje ya nchi Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sam Ellangallor aliendelea kusema “Airtel ni mtandao pekee unaotoa mawasiliano yenye uhakika zaidi kwa nchi za afrika mashariki. Airtel bado tutaendelea kuongoza kwa kutoa mawasiliano bora na  kwa gharama nafuu zaidi tukiwa tunalengo thabiti la kuondoa kabisa changamoto ya mawasiliano katika nchi za Afika Mashariki”

Maendeleo ya uchumi wa jamii huwezeshwa na muunganiko wa jitihada au nyenzo nyingi, hivyo ninaimani kuwa kuvuka kwetu mpaka na kurahisisha mawasiliano ni dhairi itasaidia kukuza na kuboresha maisha ya jamii zote. Hili imewezeshwa zaidi na wateja wanaendelea kujiunga kila siku pamoja na dhamira yetu ya kutendelea kusambaa nchi za jirani” aliongeza kusema, Sam
Posted by MROKI On Sunday, October 02, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo