Nafasi Ya Matangazo

October 03, 2011

Toka Kulia ni Afisa Biashara wa Airtel Arusha Bi Monica Ernest akikabidhi  msaada wa vitabu kwa Wanafunzi wa shule ya Ngarenaro (toka shoto) . Neema Asenga na Christina daudi wakati mgeni Rasmi Afisa Elimu Manispaa ya Arusha kwa shule za sekondari Bi. Violet Mlowosa (kati) akishuhudia. Airtel imekabidhi vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni nne vitakavyogawanywa katika shule za Olorien sekondari, Themi Sekondari, Sinoni Sekondari pamoja na Ngarenaro.makabidhiano hayo yaifanyika katika shule ya sekondari Ngarenaro Arusha.
Kushoto ni Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Airtel bw, Stephen Iketi Akyoo akikabidhi  msaada wa vitabu kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari ya Olorieni Bi. Serida Chokorera mbele ya mgeni Rasmi  Afisa Elimu Manispaa ya Arusha kwa shule za sekondari Bi. Violet Mlowosa (kati) wakati wa hafla  fupi ya makabidhiano iliyoandaliwa na Airtel katika shule ya Ngarenaro. Airtel mkoani Arusha kupitia mpango wako wa Shule yetu imekabidhi vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni nne vitakavyogawanywa katika shule za Olorien sekondari, Themi Sekondari, Sinoni Sekondari na pamoja na Ngarenaro. Mwishoni mwa wiki.
Toka Kulia ni Afisa Biashara wa Airtel Arusha Bi Monica Ernest akikabidhi  msaada wa vitabu kwa mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya Ngarenaro   Ramadhan Mshana wakati mgeni Rasmi Afisa Elimu Manispaa ya Arusha kwa shule za sekondari Bi. Violet Mlowosa (kati) akishuhudia. Airtel imekabidhi vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni nne vitakavyogawanywa katika shule za Olorien sekondari, Themi Sekondari, Sinoni Sekondari pamoja na Ngarenaro.makabidhiano hayo yaifanyika katika shule ya sekondari Ngarenaro Arusha.
*******************************************************************************
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imekabidhi  vitabu vya kiada na ziada vyenye thamani  ya shilingi milioni nne kwa shule nne za sekondari za mkoani arusha.
Hafla hiyo fupi imefanyika katika shule ya sekondari Ngarenaro huku  shule  za sekondari za Ngarenaro,Themi,Sinoni na Oloirieni zikinufzikz na msaada huo ambapo wawakilishi wa shule hizo walikabidhiwa msaada huo na meneja wa kanda ya kaskazini wa kampuni ya Airtel Tanzania bwana Stephen Akyoo.
Afisa elimu wa shule za sekondari manispaa ya Arusha  bibi Violet Mlowassa ndiye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha ambapo aliishukuru kampuni ya Airtel kwa msaada huo ambao amesema ulikuwa unahitajika na utasaidia kuboresha elimu katika shule hizo.
Kwa upande wake meneja wa Kampuni ya Airtel kanda ya kaskazini Stephen Akyoo amesema  katika kutambua umuhimu na mahitaji ya jamii ya watanzania katika kujenga taifa kupitia elimu ndio maana kampuni hiyo imekuwa na utaratibu wa kurudisha fadhila kwa watanzania kupitia Elimu.
Kwa upande wao  mkuu wa shule ya secondary Sinoni Mary Mrisho na makamu wa mkuu wa shule ya sekondari ngarenaro Eva  Mlingi wameishukuru airtel kwa msaada huo wa vitabu ambapo wametua wito kwa wanafunzi kuvitumia vizuri vitabu hivyo ika masomo yao na kutoa wito kwa makampuni na wafanyabiashara wengine kuiga mfano wa airtel .
Posted by MROKI On Monday, October 03, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo