Nafasi Ya Matangazo

April 18, 2010

Mshindi wa kwanza wa wanaume wa mbio za kilomita 15 Damian Chopa akimaliza mbio hizo wakati wa mashindano ya riadha kuchangia fedha kwa ajili ya upatikanaji wa maji maarufu kama ‘the Dow Live Earth’ katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. Mbio hizo zilidhaminiwa na Tigo, Exim Bank na wadhamini wengine.
Baadhi ya wakimbiaji wakianza mbio za kilomita 15 za kuchangia fedha kwa ajili ya upatikanaji wa maji maarufu kama ‘The Dow Live Earth’ katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. Mbio hizo zilidhaminiwa na Tigo, Exim Bank na wadhamini wengine.
Wakimbiaji wenye ulemavu wa viungo, wakianza mbio za kujifurahisha za kilomita sita pamoja na wakimbiaji wengine wakati wa mashindano ya riadha kuchangia fedha kwa ajili ya upatikanaji wa maji maarufu kama ‘the Dow Live Earth’ katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. Mbio hizo zilidhaminiwa na Tigo, Exim Bank na wadhamini wengine.
Wasanii wa kikundi cha Wakali Dancers wakitoa burudani wakati wa mashindano ya riadha kuchangia fedha kwa ajili ya upatikanaji wa maji maarufu kama ‘the Dow Live Earth’ katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. Mbio hizo zilidhaminiwa na Tigo, Exim Bank na wadhamini wengine.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya AP akitoa burudani wakati wa mashindano ya riadha kuchangia fedha kwa ajili ya upatikanaji wa maji maarufu kama ‘the Dow Live Earth’ katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. Mbio hizo zilidhaminiwa na Tigo, Exim Bank na wadhamini wengine.
Rais wa Kamati ya Paralimpiki Tanzania, Johnson Jason (kushoto) akitoa zawadi kwa mmoja wa wakimbiaji wenye ulemavu, Ernest Nabalale, mara baada ya kumalizika mbio hizo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. Mbio hizo zilidhaminiwa na Tigo, Exim Bank na wadhamini wengine. Wa pili kushoto ni Makamu wa Rais wa Riadha Tanzania, Dk Issa Ndee. Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu wa kampuni ya Tigo, Elizabeth Amayo (kulia) akitoa zawadi kwa Husna Adam wa Arusha mmoja wa washindi wa mashindano ya riadha kuchangia fedha kwa ajili ya upatikanaji wa maji maarufu kama ‘the Dow Live Earth’ katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. Mbio hizo zilidhaminiwa na Tigo, Exim Bank na wadhamini wengine. Wa pili kulia ni Meneja katika Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha Tigo, Fatma Manji
Posted by MROKI On Sunday, April 18, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo