Nafasi Ya Matangazo

April 28, 2010

Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom Tanzania, Dylan Lennox, kutokuathirika kwa mtandao wa Intanenti wa Vodacom kutokuathiriwa na tatizo la hivi hivi karibuni la mawasiliano hayo.

Na Mwandishi Wetu
Mtandao wa Intaneti wa Vodacom haujaguswa na matatizo ya intaneti nchini Wateja wa intaneti wa Vodacom Tanzania na wale wa vifurushi vya Intaneti ambayo ni makampuni makubwa hayajaathiriwa na matatizo ya intaneti yaliyoikumba nchi kwa siku kadhaa sasa.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom Tanzania, Dylan Lennox, alisema jana kwamba hali hiyo imetokana na ubora wa huduma za Vodacom Tanzania kupitia kitengo chake cha Biashara.

Kitengo hicho kimekuwa kikitoa huduma za intaneti na zile za vifurushi vya intaneti kwa kiwango cha cha juu kwa wateja wa kawaida na kwa makampuni mbalimbali.

“Wateja wetu wataendelea kupata huduma bora za Intaneti na zile za vifushi kwa uimara zaidi na kwamba hali kama hii haitatokea kwenye huduma zetu,” alisema.

Lennox alisema Vodacom Tanzania, kupitia mfumo wa 3G HSPA wenye nguvu na spidi kali inatoa huduma bora za intaneti za majumbani na zile za maofisini na kwamba wateja wenye simu pia wanazifaidi huduma hizo za intaneti.

“Kwa matinki hiyo na haya yaliyotokea hivi karibuni, maana yake ni kwamba intaneti ya Vodacom Tanzania ndiyo bora na yenye uhakika kwa sasa hapa nchini,” alisema.

Alifafanua kwamba” Siyo kwamba tunatoa huduma bora tu za intaneti, bali tunatoa huduma zenye viwango, ubora na ambazo wateja wetu wanaweza kuzimudu,”.

Alisema Kitengo chake ni suluhisho ya mahitaji ya intaneti kwa makampuni makubwa na kwamba hivi karibuni kitazindua huduma nyingine zaidi ambazo zitatoa wigo mpana kwa huduma za intaneti na vifurushi vya intaneti kwa makampuni makubwa.

“Tutaendelea kutoa huduma bora na kwamba wateja wetu kwamwe hawawezi kupata matatizo kutokana na kuharibika kwa njia za mawasiliano za baharini kama ilivyotokea kwa sasa, kwa kweli, Vodacom iko juu,” alisema.
Posted by MROKI On Wednesday, April 28, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo