Nafasi Ya Matangazo

April 28, 2010

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya Marehemu Evaristi Semeni mtoto mwenye umri wa miaka 11 kumi na moja aliyefariki katika ajali ya kugongwa na gari juzi jioni katika kijiji cha Msoga ambapo yeye pamoja na watoto wengine wawili walifariki dunia.Semeni alikuwa mwanafunzi katika shule ya msingi Msoga.Semeni pamoja na wenzake Ezekiel George Setumbi(13) mwanafunzi katika shule ya msingi Mboga wilayani Bagamoyo na Omari Mrisho aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Msoga walifariki dunia baada ya kugongwa juzi saa moja na nusu jioni na lori aina ya Isuzu Tiper lenye usajili wa namba SM 2514 mali ya Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo lililokuwa likitoka Chalinze Kuelekea Msata.Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Bwana Mohamed Mbwana amesema kuwa wakati wa ajali hiyo mtoto Ezekiel Setumbi alifariki papo hapo ambapo wenzake Evarist Semeni(11) na Omari Mrisho(13) walifariki wakati wakipata matibabu katika kituo cha afya Chalinze. Kwa Mujibu wa Kamanda Mbwana Dereva wa lori hilo Lukino Kayela(40) mkazi wa Mji Mwema Bagamoyo amekamatwa na alitarajia kufikishwa mahakamani leo.Wanafunzi hao walifariki kutokana na majeraha makubwa waliyoyapata kichwani.Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika nyumba ya familia ya Marehemu Evaristi Semeni(11) mmoja kati ya watoto watatu walifariki kwa ajali ya kugongwa na lori katika kijiji cha Msoga wilayani Bagamoyo,juzi jioni.Rais Kikwete alizitembelea familia za marehemu na kuwafariji jana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwafariji baadhi ya wakazi wa vijiji vya Msoga na Mboga wilayani Bagamoyo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mzee Mrisho Omari mzazi wa Marehemu Omari Mrisho(13) katika kijiji cha Msoga jana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifika kutoa heshima za mwisho na kuifariji familia ya marehemu Omari Mrisho(13) aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya msingi Msoga ambaye yeye na wanafunzi wenzake wawili walifariki katika ajali ya gari iliyotokea katika kijiji cha Msoga juzi.

Posted by MROKI On Wednesday, April 28, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo