Nafasi Ya Matangazo

March 29, 2010


Ziara ya Mke Rais, Salma Kikwete leo iliingia dosari baada ya magari mawili kupata ajali wakati wakikwepa lori lililokuwa barabarani.

Ajali hiyo ilitokea saa 3:00 asubuhi katika daraja la Kirume mpakani mwa wilaya ya Musoma na Rorya mkoani Mara wakati msafara huo ukielekea wilayani Tarime.
Baada ya ajali hiyo, msafara ulilazimika kusimama kwa muda mfupi na baadae kuendelea kama kawaida, ingawaje hakuna aliyejeruhiwa, isipokuwa magari mawili yaliyokuwa kwenye msafara kuharibika.

Katika magari yaliyoharibika, mojawapo lilikuwa limebeba waandishi wa habari na lingine halikufahamika mara moja ambapo lori lililosababisha ajali lilitokea njiani likitokea Tarime Taarifa ambazo hazijathibithibitishwa lori hilo liko mikononi mwa polisi.

Wakati huohuo, GARI ya polisi imepoteza mwelekeo na kuwajeruhi vibaya watu wanne akiwamo mwanafunzi wa shule ya Sekondari eneo la Tarime Mjini, mkoani Mara.

Waliojeruhiwa katika tukio hilo lililotokea jana asubuhi wametambuliwa na ni Nyamahende Msolwa, Mwita Mohere, Wangwe Magere na Agnes Joseph ambaye ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Nkendeiliyopo nje kidogo ya mji wa Tarime.

Majeruhi wote walikimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Tarime kwa ajili ya matibabu.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika katika hospitali hiyo, mwanafunzi huyo na watu wengine wawili waliojeruhiwa katika ajali hiyo wamevunjika miguu vipande vipande.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo Polisi wa Usalama wa barabarani aliyewasili katika eneo la tukio baada ya ajali kutokea, alivamiwa na wananchi wenye hasira ambao walimrushia mawe.

Mashuhuda hao waliodhani kuwa majeruhi hao wanne wote wamekufa lakini kwa mujibu wa ripoti kutoka kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Tarime Constantine Masawe alisema watu hao hawajafa ila wamejeruhiwa.

“Mpaka sasa hakuna mtu aliyekufa na madaktari wanafanya kila jitihada kuokoa maisha ya majeruhi hao.” Alisema Massawe alipozungumza na HabariLeo kwa njia ya simu muda mfupi baada ya tukio hilo.

Ofisa Mpelelezi wa Mkoa (RCO), David Hiza, alikuwa ni mmoja wa maofisa wa polisi ambap walikimbilia hospitalini hapo kuhakikisha majeruhi hao wanapatiwa huduma.

“Wote wanapumua na madaktari wanafanya kazi yao, tuwape muda,” alisema RCO huyo alipokuwa hospitalini hapo.

Ajali hiyo ilitokea wakati, Mke wa Rais, Salma Kikwete akitarajiwa kuhutubia katika mkutano wa wananchi Tarime mjini ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika Kanda ya Ziwa.

Inadaiwa ajali hiyo ilitokea baada ta dereva aliyekuwa anaendesha gari ya polisi kugonga sehemu ya gari lingine lililokuwa linaendeshwa na mmoja wa wafanyabiashara maarufu katika eneo hilo.
Posted by MROKI On Monday, March 29, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo