Nafasi Ya Matangazo

March 31, 2010

Kundi zima la Mashujaa Musica.
Bendi mpya ya muziki wa dansi nchini MASHUJAA BAND, imewaandalia Burudani ya aina yake siku ya Sikukuu ya Pasaka katika ukumbi wa Bwalo la Magereza ambapo pia kutakuwa na Bonanza la aina yake litakaloshirikisha timu mbalimbali za maveterani kutoka mikoani.

Kwa mujibu wa Shaaban Mpalule msemaji wa bendi hiyo burudani itaanza saa tisa mchana ambapo nyimbo mbalimbali zitatumbuizwa ikiwa ni pamoja na kutambuylishwa nyimbo mpya inayotazamiwa kurekodiwa mara tu baada ya Sikukuu ya Pasaka ya Safari yenye Vikwazo mtunzi Jadol Fidifosi (FFU).

Aidha bendi hiyo siku ya leo ipo Woodland kwa jimmy Yombo, kesho itakuwa katika ukumbi wake wa nyumbani wa Mashujaa Pub, ijumaa itatelemka katika ukumbin wa Equatol Grill Temeke Mtoni, jumamosi itafanya onyesho tena katika ukumbi wa Woodland, jumapili itashuka kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Magereza Ukonga.

Katika Maonyesho hayo wanamuziki na Wacheza shoo wote nyota wa kundi hilo watakuwapo, ikiwa ni pamoja na Kiongozi wa bendi Aliston Angai, Despino Malaika, Geran Kissa, Masooud USB, Ngosha Mwanamasanja, Jado Fidifosi, Pasia Budansi, Raja Rado, na wengine wengi.

Kwa upande wa Burudani ya Shoo bendi hiyo imezidi kung’ara zaidi kutokana na juhudi za Sharony Mapozi, Frida Mwanasuka, Sarafina Shotii,Pendo Bonzo, Merisa Maga, pamoja na Etoo Tisa.

Wengine ni mpiga gitaa, Amosi Ras, Baba , Flora Bambucha, Sarafina Shotii, Sharoni Mapozi, Neema Mkama, Pendo Boza, Frida Etoo Tisa, huku waimbaji wakiwemo Ibrahimu Milinda Nyeusi, Pasia Budansi Bakiza Mambo(Raja), Desipino Malaika, Masoud USB, Edward Anthony MaliKidogo(jadol Feed Force FFU) na Mwanamuziki na rapper wa bendi SIMONG NGOSHA(ngosha masanja)

Nyimbo zinazovuma kwa sasa ni ule wa Mwanike ulioimbwa kwa mchanganyiko wa makabila ya Kisukuma na Kihaya, ukiwa umetungwa na Ngosha Mwanamasanja na Moshi wa Sigara uliotungwa na mwanamuziki Pasia Budansi.

Viingilio katika maonyesho yote ni vya kuridhisha ili kuwapa mwanya wote kwenda kushuhudia bendi hiyo mpya ya nyumbani inavyokuja kwa kasi katika medani ya muziki wa dansi.
Posted by MROKI On Wednesday, March 31, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo