Nafasi Ya Matangazo

March 21, 2010

Baadhi ya Watanzania waishio Namibia wakimlaki kwa furaha Rais Jakaya Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili nchini humo kuhudhuria sherehe za miaka 20 ya Uhuru wa nchi hiyo ambapo pia Rais wa nchi hiyo Hifikepunye Pohamba ataapishwa kuendelea kuingoza nchi hiyo katika muhula wa pili kama Rais.
Watanzania waishio Namibia wakimsalimia Rais Kikwete.
Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia akimtunuku Nishani ya Juu ya Ushujaa ya Taifa la Namibia Rais Mstaafu wa Zambia Kenneth Kaunda kwa kutambua mchango wake katika ukombozi wa nchi za kusini Mwa Afrika ikiwemo taifa la Namibia.
Rais Wa Namibia Hifikepunye Pohamba akimkabidhi Nishani ya Juu ya Ushujaa ya Taifa la Namibia, Mama Maria Nyerere kwa niaba ya Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa kutambua juhudi za Mwalimu katika ukombozi wa bara la Afrika ikiwemo Namibia katika hafla maalumu iliyofayika katika mji mkuu wa nchi hiyo Windhoek jana jioni.Katika hafla hiyo viongozi Mbalimbali wa Afrika waliokuwa mstari wa mbele katika harakati za ukombozi kusini mwa Afrika nao walitunukiwa nishani hiyo akiwemo Rais wa Zamani wa Zambia Keneth Kaunda ambaye pia alihudhuria hafla hiyo, Marehemu Agostino Neto wa Angola, Marehemu Oliver Tambo wa Afrika ya Kusini, Rais Denis Sassou Nguesso wa Kongo Brazaville, pamoja na watu wengine mashuhuri waliokuwa msari mbele katika ukombozi wa bara la Afrika.Pembeni ya Mama Maria kushoto ni Mtoto wa Mwalimu,Bwana Makongoro Nyerere ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mara.
Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Rais wa Namibia Hifikepunye Pohamba katika hafla maalumu kuadhimisha miaka 20 ya Uhuru wa Namibia na pia kushinda uchaguzi mkuu ambapo ataendelea kuiongoza Namibia kwa muhula wa pili.Sherehe hizo zilifanyika katika mji mkuu wa Namibia Windhoek jana.
Posted by MROKI On Sunday, March 21, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo