Nafasi Ya Matangazo

December 25, 2008

Bi Mariam Rajabu Mkazi wa Mwanayamala A Dar es Salaam nimiongoni mwa akina dada waliojaliwa watoto katika mkesha wa Krismasi. Mariam amejifungua mapacha wa tatu katika Hospitali ya Mwananyamala na yupo katika mtijhani mzito wa juu ya kuwalea watoto hao watatu ambao mmoja kati yao ni wakike. Kwamuji wa Mariam anasema aliyempa ujaziuzito huo alimkana tangu mwanzo na hamjali kwa lolote na Familia anayoishi nayo pia ni maskini. Na tangu amelazwa hapo hakuna yeyote aliyefika kumjulia hali na anategemea msaada mkubwa wa wauguzi. Anaomba yeyote aliye na msaada wa hali na mali chakula au mavazi asisite mkusaidia ili kumpunguzia ugumu wa kulea viumbe hivyo visivyo na hatia vilivyozaliwa katika kumbukumbu ya kuzaliwa Kristo Yesu au Nabii Isa.
Yeyote mwenye chochote awasiliane nami na tutamsaka dada huyu na msaada umfikie.
Posted by MROKI On Thursday, December 25, 2008 1 comment

1 comment:

  1. Pole dada MUNGU atakusaidia kukuza wanao.Swali kwa wasomaji wote,Mi najua pacha ni kwa vitu viwili,watoto tunaita hivyo wakizaliwa wawili kwa mpigo.sasa wamezaliwa watoto watatu kwa kiinglishi mie nadhani wanaitwa triplets.kiswahili sijui inatafsiriwaje ila MAPACHA ni wakiwa wawili.Anayejua tasfiri yao nitashukuru kupewa mwanga katika hili.

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo