Nafasi Ya Matangazo

December 25, 2008

Mtoto huyu mkazi wa Dar es Salaam alikuwa akiwashangaza wengi katika fukwe ya Coco Beach leo kwa umahiri wake wa kufakamia ze Mbuyu (Safari) bila kutikisika. Kwa mujibu wa mama yake mdau huyu huondoka kilaji hadi mbili na yupo fiti.
Ingawaje mzazi alionyesha kufurahia unywaji huo wa mtoto lakini Blog hii inawaonya wazazi wote wenye tabia kama hii kuacha mara moja kwani inaharibu watoto. Mama wa mtoto huyo akiwa na safari zake
Dogo akiendeleza libeneke


Posted by MROKI On Thursday, December 25, 2008 9 comments

9 comments:

  1. Bro..mimi napenda sana blog yako..ukweli ni kuwa unatoa picha halisi ahsante

    It is me Alvin from Houston Texas

    ReplyDelete
  2. She should be arrested!

    ReplyDelete
  3. Nikiwa kama mzazi nakemea hii tabia kwa nguvu zote. Alcohol ni chemicals ambazo zinaweza haribu kidney, liver kwa mtoto kama huyo. Na sio hivyo tu alcohol abuse ni addiction na itamuharibia maisha yake. Sijui taratibu za serekali yetu zikoje lakini nadhani kuna idara kama za ustawi wa jamii ambazo zingekuwa responsible kuhakikisha mtoto anapata malezi yanyostahili. Kama baba ya mtoto naye hawezi kuingilia kati angalu basi mtoto anweza kabidhiwa kwa ndugu na jamaa mfano bibi na babu yake. Lakini mzazi huyu anatakiwa kuchukuliwa hatua. Kuna makabila mengine yanaidhinisha unywaji pombe kwa watoto but not at this level. This needs to be stopped.

    ReplyDelete
  4. HIVI NDIO VITU VYA KUKEMEA KWA NGUVU ZOTE UJINGA NA UPUMBAVU WA HIVI UNAONYESHA NI JINSI GANI BAADHI YA WAZAZI WAKIWA HAWAJUI WAJIBU WAO SI TU KWA WATOTO BALI KWA JAMII NZIMA.
    HUWEZI JUA LABDA ALIPATIKANA KWENYE KILAJI HUYU MTOTO

    ReplyDelete
  5. MAMA MWENYEWE ANAONEKANA SI RIZIKI, UNATEGEMEA MWANAE AWEJE, NDO TANZANIA TUNAYOJENGA. MUULIZE MTOTO ATAKWAMBIA ANFAHAMU HATA VIWANJA VYA STAREHE ,PIA BAR ZA DAR.
    SHUJAA WA MTOTO NI WAZAZI.

    ReplyDelete
  6. SERIKALI HIVI IKO WAPI??? TUNAISHAI BILA SHERIA NCHI HII,SASA MAMA KAMA HUYU HAJASHTAKIWA WALA KUNYANG'ANYWA MTOTO! TUNAOMBA WAHUSIKA WAMSHTAKI MAMA WA MTOTO HUYU KWA SABABU HII SIO KAWAIDA NA NI KOSA LA JINAI,KAMA ANAMRUHUSU KUNYWA POMBE HII INAONYESHA KUWA BASI MTOTO HUYU ANAFANYA ZAIDI YA HAYO KUPITIA MAMA YAKE.

    ReplyDelete
  7. BLOG NYINGINE MNABOA,PICHA WIKI NZIMA???????????????????JIFUNZENI KWA MICHUZI,HUWA TUNATEMBELEA BLOG ZENU ILA HAZINA CONTENTS NA NEW THINGS,HAMBADILIKI???????MBONA KUWASHIKA WATU NI KITU KIDOGO,HALAFU CHA AIBU ZAIDI NINYI NI WAANDISHI WA HABARI,MBONA MNATIA AIBU NA KAZI ZENU,NI WAANDISHI GANI MSIEJUA KUWA FLESH NEWS NDIO ZINAUZA?????????WATU WANATAKA VITU VIPYA.MNAONYESHA JINSI GANI NI VIHIYO KWENYE FANI HIYO.KAMA HAMUWEZI ACHENI!!!!!!!!!!!!!
    MDAU UGHAIBUNI.

    ReplyDelete
  8. Anachokifanya huyo mama ni kosa kubwa, kwanza kwa kawaida pombe haziruhusiwi kwa mtoto chini ya miaka kumi na nane, japokuwa huwa tunarahisisha mambo mengine. Ninavyofahamu mimi ni kwamba kuna sheria zinazomlinda mtoto dhidi ya uharibifu kama huu. hii inaonyesha wazi kwamba huyo mtoto alipatikana katika mazingira ya ofa za pombe, na mamake amekuwa akiendelea na mchezo huo. Napata hisia kabisa kwamba huyo mama amekuwa akimpa pombe mwanae kama njia mojawapo ya kumfanya au alale ili yeye atoke na kwenda kustarehe, au akiwa kwenye starehe amekuwa akimpa pombe ili alale na yeye apata nafasi ya kuendelea na anasa zake, au wakati mwingine hata nyumbani inawezekana mama ni mtu wa kubadilisha wanaume, na nji ya kufurahia uhuni wake ni kumfanya mtoto alale kwa pombe na matokeo yake ndio hayo mtoto anakuwa sugu kwa pombe. katika mazingira ya kawaida haiwezekani mtoto mdogo kama huyo awe na uwezo wa kunywa bia zaidi ya moja tena safari lager. Huyo mama atakuja kujuta baadae kwa hilo analolifanya, labda asifikie kumshuhudia mwanae akiwa mtu mzima, atajuta sana. na serikali/ watu walio karibu wanaofahamu udhalimu huo dhidi ya huyo mtoto wangeweza kufanya jambo, maana serikali haipiti mitaani kutafuta nani anafanya nini nyumbani kwake, ni wajibu wetu kuisaidia kuwabaini watu kama hao, nina hakika huyo mama akiripotiwa katika vyombo vya dola vitamshughulikia, sisi tunasema na kulaumu kwa vile tumeiona picha, hivyo basi tumpeleke kunakohusika. Ana bahati nipo mbali ningeshughulikia hili mpaka kieleweke.

    Pia mkuu wa hii blog, rekebisha mambo, unaweka habari moja muda mrefu sana utadhani sio mwandishi wa habari mkuu, inabore sana unapoingia mtandaoni na kukuta habari ile ile kila siku.

    ReplyDelete
  9. MDAU PUNGUZA HASIRA DUH!! ILA UNACHOSEMA NI KWELI KAKA

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo