Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Brig. Jen Hosea Ndagala akieleza kuhusu utekelezaji wa shughuli za maafa kwa nchi ya Tanzania kwa timu ya uongozi wa Wilaya ya Mapai iliyopo Mkoa wa Gaza Nchini Msumbiji walipotembelea kujionea moja ya mradi wa kuwezesha wananchi kuwa na vitalu nyumba vinavyotumika kwa shughuli za kilimo kwa lengo la kukabiliana na athari za majanga ikiwemo mafuriko na ukame,wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Utawala wa eneo la Mapai Mhe. Maria Helena Coreia Langa.
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Brig. Jen Hosea Ndagala akizungumza jambo na wanakikundi wanaonufaika na mradi wa vitaru nyumba (Gree House) vinavyotumika katika masuala ya menejimenti ya maafa kwa shughuli za kilimo cha mazao mbalimbali ili kuendelea kukabiliana na maafa na kurejesha hali.Timu kutoka Tanzania wametembelea eneo la Mapai ikiwa ni sehemu ya ziara ya kubadilishana uzoefu kati ya Tanzania na Msumbiji kuhusu hatua za mapema kabla ya majanga kutokea.
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Brig. Jen Hosea Ndagala (katikati mwenye shati nyeupe) pamoja na Mkuu wa Utawala wa Wilaya ya Mapai Mhe. Maria Helena Coreia Langa (katikati mwenye blauzi nyekundu na kilemba) wakiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Tanzania uliotembelea kujionea miradi ya kuwezesha wananchi katika kukabiliana na majanga pamoja na athari za maafa ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kubadilishana uzoefu kati ya Tanzania na Msumbiji kuhusu hatua za mapema kabla ya majanga kutokea.
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Brig. Jen Hosea Ndagala akizungumza jambo na wanakikundi wanaonufaika na mradi wa vitaru nyumba (Gree House) vinavyotumika katika masuala ya menejimenti ya maafa kwa shughuli za kilimo cha mazao mbalimbali ili kuendelea kukabiliana na maafa na kurejesha hali.Timu kutoka Tanzania wametembelea eneo la Mapai ikiwa ni sehemu ya ziara ya kubadilishana uzoefu kati ya Tanzania na Msumbiji kuhusu hatua za mapema kabla ya majanga kutokea.
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Brig. Jen Hosea Ndagala (katikati mwenye shati nyeupe) pamoja na Mkuu wa Utawala wa Wilaya ya Mapai Mhe. Maria Helena Coreia Langa (katikati mwenye blauzi nyekundu na kilemba) wakiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Tanzania uliotembelea kujionea miradi ya kuwezesha wananchi katika kukabiliana na majanga pamoja na athari za maafa ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kubadilishana uzoefu kati ya Tanzania na Msumbiji kuhusu hatua za mapema kabla ya majanga kutokea.
Mkuu wa Utawala wa eneo la Mapai Mhe. Maria Helena Coreia Langa akizungumza jambo na wanakikundi wanaonufaika na mradi wa vitalu nyumba (Gree House) vinavyotumika katika masuala ya menejimenti ya maafa kwa shughuli za kilimo cha mazao mbalimbali ili kuendelea kuwa na ustahimilivu wakati wa maafa na kurejesha hali.Ujumbe kutoka Tanzania wametembelea eneo la Mapai ikiwa ni sehemu ya ziara ya kubadilishana uzoefu kati ya Tanzania na Msumbiji kuhusu hatua za mapema kabla ya majanga kutokea.
Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Brig. Jen Hosea Ndagala akieleza namna Tanzania inavyosimamia masuala ya maafa wakati wa kikao cha pamoja na uongozi wa Wilaya ya Mapai iliyopo mkoa wa Gaza nchini Msumbiji wakati wa ziara ya kujionena namna wanavyoratibu na kusimamia masuala ya maafa ikiwa ni sehemu ya ziara ya kubadilishana uzoefu kati ya Tanzania na Msumbiji kuhusu hatua za mapema kabla ya majanga kutokea.
Mratibu wa Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Kapteni Emmanuel Lyimo akiuliza swali kwa uongozi wa Wilaya ya Mapai wakati wa kikoa cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa masuala ya maafa walipotembelea ikiwa ni sehemu ya ziara ya ziara ya kubadilishana uzoefu kati ya Tanzania na Msumbiji kuhusu hatua za mapema kabla ya majanga kutokea.Kikao kimefanyika Ofisi za Wilaya ya Mapai mkoani Gaza Nchini Msumbiji.
Kiongozi wa Hatua za Kutarajia na Usimamizi wa Maafa kutoka Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bi. Sandra Hakim akifafanua jambo wakati wa kikoa cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa masuala ya maafa katika Wilaya ya Mapai walipotembelea ikiwa ni sehemu ya ziara ya ziara ya kubadilishana uzoefu kati ya Tanzania na Msumbiji kuhusu hatua za mapema kabla ya majanga kutokea.Kikao kimefanyika Ofisi za Wilaya ya Mapai mkoani Gaza Nchini Msumbiji.
*************
Na, Mwandishi wetu, Mapai - MsumbijiTANZANIA imeendelea kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha udhibiti wa maafa unaanzia ngazi ya chini ya jamii, hatua inayolenga kuongeza ufanisi katika tahadhari, maandalizi na mwitikio wa haraka pindi majanga yanapotokea.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Brigedia Jenerali Hosea Ndagala, walipotembelea Wilaya ya Mapai iliyoko mkoa wa Gaza Nchini Msumbiji ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kubadilishana uzoefu kati ya Tanzania na Msumbiji kuhusu hatua za mapema za kukabiliana na majanga.
Amesema moja ya mambo makubwa yakujivunia ni namna mifumo ya usimamizi wa maafa ilivyoimarika kuanzia ngazi ya chini jambo linalosaidia kuongeza ufanisi na mwitikio wa haraka pindi majanga yanapotokea.
Aidha, akieleza faida ya ziara hiyo Wilayani Mapai ni kuchukua uzoefu wa namna ya kuongeza tija katika eneo la kurejesha hali na kukabiliana na maafa kwa kuwa na miradi ya kutosha inayosaidia jamii kuwa na mwendelezo wa hatua za kuchukua kabla ya majanga, huku akipongeza miradi inayotekelezwa katika eneo hilo ya ujenzi wa Vitalu nyumba vinavyotumika kwa shughuli za kilimo cha mazao mbalimbali ili kusaidia kuwa na jamii stahimilivu dhidi ya majanga.
“Tumeshuhudia jinsi serikali ya Msumbiji ilivyojipanga kuanzia ngazi ya jamii katika kukabiliana na maafa kwa kuwa na miradi mbalimbali ikiwemo ya Vitalu nyumba.Hii ni hatua muhimu ambayo Tanzania tunaenda kuiboresha zaidi,” amesema Brig Jen.Ndagala.
Vilevile, amesema kuwa kwa upande wa Tanzania, juhudi kama hizo tayari zimeanza kuzaa matunda, ikiwemo ujenzi wa nyumba kwa waathirika wa maporomoko ya mawe na tope kutoka Mlima Hanang' mkoani Manyara, hatua iliyosaidia kurejesha matumaini kwa wananchi.
Kwa Upande wake Mkuu wa Utawala wa Wilaya ya Mapai Mhe. Maria Helena Coreia Langa amepongeza ziara hiyo muhimu kwa wilaya yake kwa kuzingatia umuhimu na matokeo chanya yatakayoimarisha uhusiano ya nchi hizo mbili kwa kuzingatia lengo kuu la kubadilishana uzoefu kati ya nchi hizo mbili kuhusu hatua za mapema kabla ya majanga kutokea.
“Tutaendelea kuongeza ubunifu katika hatua za kukabiliana na maafa katika maeneo yetu kwani tumekuwa tukikubwa na vimbunga, mafuriko na ukame mara kwa mara, hii ni hatua muhimu ya kupeana uzoefu ili kuimarisha mifumo yetu na kuwa na jamii stahimilivu dhidi ya majanga,” alisema Mhe. Maria
Aliongezea kuwa,hatua ya Tanzania kuja kujifunza na kupeana uzoefu imewapa darasa kwa namna Tanzania inavyoratibu maafa kwa kutumia mifumo ya TEHAMA na matumizi ya Akili Unde katika usimamizi wa shughuli za maafa.
“Ninawapongeza kwa namna mnavyoendelea kuweka mifumo thabiti ya kukabiliana na athari za majanga pamoja na mifumo ya tahadhari za mapema na ile ya uwepo wa Kituo cha Kitaifa cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura (EOCC) kinachorahisisha Mfumo wa Taarifa wa Usimamizi wa Maafa (e-MAAFA) hakika hii ni hatua nzuri, katika masuala yetu ya kusimamia maafa,” alieleza Mhe. Maria
Akieleza historia ya eneo la Mapai amesema limekuwa likikabiliwa na mafuriko makubwa ya mara kwa mara yanayosababishwa na mvua kubwa, vimbunga, na kuongezeka kwa maji ya mito (kama vile Mto Limpopo), ambayo mara kwa mara huiacha wilaya ikiwa imetengwa kwa kiasi kikubwa, kuharibu barabara, na kutishia usalama wa chakula wa ndani.













0 comments:
Post a Comment