Nafasi Ya Matangazo

May 29, 2026


Dodoma
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imeendelea na utekelezaji wa Mpango wa Ununuzi wa Dhahabu wa Ndani (Domestic Gold Purchase Programme - DGPP) ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuimarisha sekta ya madini na kuongeza mchango wa dhahabu katika uchumi wa taifa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Leseni wa Tume ya Madini, Eng. Aziza Swedi kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Eng. Ramadhani Lwamo, BOT imeidhinisha kiwanda cha kusafisha dhahabu cha SABGOLD Limited Refinery kilichopo Kahama, Mkoa wa Shinyanga kuwa mojawapo ya vituo rasmi vya kupokea na kusafisha dhahabu kwa ajili ya ununuzi wa BOT.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kituo hicho kitaanza rasmi kutoa huduma kuanzia Mei 30, 2026, hatua inayotarajiwa kuongeza ufanisi katika biashara ya dhahabu pamoja na kuwapa wachimbaji na wafanyabiashara fursa ya kuuza dhahabu yao kupitia mfumo rasmi na wenye tija zaidi.

“Tume ya Madini inapenda kuujulisha umma, wachimbaji, wafanyabiashara wa madini pamoja na wadau wote wa sekta ya madini kuwa BOT inaendelea na utekelezaji wa mpango huu muhimu kwa maendeleo ya sekta ya madini nchini,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, wadau wametakiwa kuwasiliana na Dkt. Anna Lyimo kupitia namba +255 756 389 128 au Bw. Joshua Maganga kupitia +255 675 995 014 kwa maelezo zaidi kuhusu taratibu za mpango huo.
Posted by MROKI On Friday, May 29, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo