Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini MHE. DANIEL BARAN SILLO amechaguliwa na Wabunge kushika nafasi ya Naibu Spika wa Bunge.
Uchaguzi wa Mhe. Sillo ulifanyika muda mfupi baada ya kuthibitishwa na Bunge kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mwigulu Nchemba.
Sillo amechaguliwa kwa kura za ndio 371 kati ya kura 371 zilizopigwa na Wabunge.
Tayari Naibu Spika ameshakula Kiapo cha kushika nafasi hiyo na anataraji kufanya mahojiano na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuahirishwa kwa kikao cha Bunge hii leo Novemba 13, 2025 katika lango kuu la kuingilia bungeni.





0 comments:
Post a Comment