Nafasi Ya Matangazo

March 03, 2026

 





Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesogeza karibu huduma za Sekta ya Ardhi kwa wanawake nchini nchini kupitia Kliniki ya Ardhi Maalumu "Samia Ardhi Kliniki"

Mkoa wa Simiyu ni miongoni mwa mikoa ambayo Kliniki hiyo inaendeshwa ambapo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi Machi 4, 2026 na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anamringi Macha katika Viwanja vya Sabasaba vilivyopo katika mji wa Bariadi.

Katika kufanikisha Kliniki hiyo, Wizara na Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Simiyu inashirikiana na team ya wataalamu wa Sheria kutoka Mama Samia Legal Aid kutoa huduma za Sekta ya Ardhi ikiwemo upimaji wa ardhi, utoaji wa Hati Miliki, uhamishaji wa umiliki, uthamini wa ardhi, kusikiliza changamoto mbalimbbali za sekta ya ardhi na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu matumizi bora ya ardhi.

Kliniki hiyo inalenga kutoa huduma za ardhi kwa wanawake nchi nzima kuelekea Siku wa Kimataifa ya Wanawake kuanzia tarehe 2 hadi 7 Machi 2026 ikiongozwa na Kaulimbiu "Haki sawa kwa Wanawake na Wasichana; Msingi Jumuishi kifikia Dira 2050"
Posted by MROKI On Tuesday, March 03, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo