September 02, 2025

DKT.NCHIMBI AWANADI WAGOMBEA UBUNGE,MADIWANI WA SIMIYU KWA WANANCHI




MGOMBEA mwenza wa kiti cha urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Balozi Dkt.Emmanuel  John Nchimbi 
amepokelewa kwa shangwe na wananchi alipokuwa akiwasili katika uwanja wa CCM,wilaya ya Bariadi Vijijini  mkoani Simiyu kuendelea na mkutano wa Kampeni, leo Jumatatu Septemba 1,2025.

Dk.Nchimbi aliyekuwa Mkoa wa Mara na sasa ameingia Mkoa wa  Simiyu kuendelea na kampeni,akianzia jimbo la Busega na baadae kuelekea  jimbo la Bariadi Vijijini na kufanya mikutano mikubwa ya hadhara.
 
Akiwahutubia wananchi wa Bariadi Vijijini  mkoani Simiyu, Dkt.Nchimbi ambae ni Mgombea Mwenza wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, pia alimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi Vijijini,Masanja  Kungu Kadogosa sambamba na wagombea ubunge wengine pamoja na Madiwani wa mkoa huo.

Dkt. Nchimbi anaendelea na kampeni zake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, ikiwa ni katika harakati za kuomba ridhaa ya Watanzania  kuwaongoza katika awamu nyingine ya miaka mitano, katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa Kufanyika Oktoba 29, 2025.





No comments:

Post a Comment