Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Samia Suluhu Hassan amesema ndani ya Siku 100 atakapoingia Madarakani, Serikali ya Chama hicho, itaanza kugharamia matibabu ya magonjwa yanayowatesa Watanzania, ikiwemo Saratani pamoja na Figo.
Kauli hiyo imetolewa Septemba 01, 2025 na Mgombea mwenza wa Urais wa CCM, Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi alipowasili katika kata ya Mkula, Wilaya ya Busega mkoani Simiyu kwa ajili ya kunadi Sera na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2025-2030.
MGOMBEA Mwenza wa kiti cha urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Emmanuel Nchimbi amepokelewa kwa shangwe na Wananchi wa wilaya ya Busega,wakati alipokuwa akiwasili katika uwanja wa shule ya Msingi Mkula,Busega mkoani Simiyu kuanza mikutano ya Kampeni katika mkoa huo leo Jumatatu Septemba 1,2025.
Dk.Nchimbi alikuwa mkoa wa Mara na sasa ameingia mkoa wa Simiyu kuendelea na kampeni katika Mkoa huo,ambapo ameanza na jimbo la Busega.
Akiwahutubia wananchi wa Busega mkoani Simiyu, Balozi Dkt.Nchimbi alisema Serikali ya CCM chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imejipanga kuuletea maendeleo zaidi mkoa wa Simiyu.













No comments:
Post a Comment