Nafasi Ya Matangazo

August 31, 2025



Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi leo Jumapili Agosti 31 ,2025 ameendelea na kampeni zake kwa kufanya mkutano mkubwa katika mji wa Nyamongo, jimbo la Tarime vijijini mkoani Mara.

Balozi Dkt.Nchimbi  pia aliwanadi wagombea Wabunge wa majimbo ya Mkoa huo akiwemo  mgombea Ubunge wa Jimbo la Tarime Vijini,Mwita Waitara Pamoja na  Madiwani

Dkt.Nchimbi ameanza kampeni zake mkoani Mara jana Agosti 30, 2025 akitokea mkoa wa Mwanza, ikiwa ni katika harakati za kuomba ridhaa ya Watanzania  walioko Kanda ya Ziwa katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa Kufanyika Oktoba 29, 2025.










Posted by MROKI On Sunday, August 31, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo