Maeneo mengine ni pamoja na elimu ya mifugo, kilimo na Uvuvi kupitia programu ya Kuendeleza ya kilimo na uvuvi (AFDP) pamoja na Program ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II).
Watalaam hao wanawake kutoka katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) wameonekana wakitoa elimu hiyo kwa makundi mbali mbali ya wanawake wasichana na vijana wa rika tofauti leo Tarehe 07 Machi 2025 na kuendelea.
Maadhimisho hayo yanatanguliwa na Kaulimbiu inayosema "Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji".
Aidha katika kuadhimisha kilele ya siku hiyo,Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment