Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.
Jaji wa Rufani (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifunga mafunzo
ya siku mbili ya watendaji wa uboreshaji wa Daftari kutoka halmashauri zote za
mkoa wa Dar es Salaam leo Machi 07,2025.
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku mbili ya watendaji wa uboreshaji wa Daftari kutoka halmashauri zote za mkoa wa Dar es Salaam leo Machi 07,2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akifafanua jambo.
Washiriki wa Mafunzo hayo wakifuatilia Hotuba ya kufunga mafunzo hayo
Na. Mwandishi Wetu, Dar es SalaamTume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewataka watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwahamasisha wananchi wenye sifa ili wajitokeze kujiandikisha na kupata haki yao ya kikatiba itakayowawezesha kushiriki katika kuchagua viongozi wao.
Jaji Mbarouk amewaasa kuwa licha ya shughuli nyingi za kiutendaji walizonazo watendaji hao wafuatilie kwa karibu zoezi hilo na kushiriki kikamilifu ili kuhakikisha kuwa linafanikiwa.
No comments:
Post a Comment