Mkutano baina ya na Mhe. Rais Azali Assoumani wa Umoja wa Visiwa vya Comoro na Balozi wa Tanzania Nchini Comoro, Mhe.Balozi Said Yakubu umefanyika ambapo mengi ya faida baina ya Tanzania na Comoro yamejadiliwa.
Mhe.Rais Azali amepongeza juhudi za Serikali ya Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuongeza ushirikiano wa kibiashara baina ya Tanzania na Comoro ambapo katika kipindi cha Julai mpaka Desemba kumekuwa na makongamano ya wafanyabiashara katika sekta za Kilimo,Mifugo na Usafirishaji na pia Kambi ya Matibabu iliyowasaidia wananchi wa Comoro.
Aidha,Mhe.Rais Azali pia ameeleza azma ya Serikali yake kuanza kufundisha lugha ya Kiswahili mashuleni kufuatia maombi yaliyowasilishwa awali na Serikali ya Tanzania kupitia Ubalozi na kuelekeza mazungumzo rasmi yaanze kwa ajili ya mahitaji ya walimu na vifaa husika.
Katika mkutano huo,Balozi Yakubu alimkabidhi Rais Azali jezi ya Timu ya Taifa ya Tanzania yenye jina lake kama zawadi ya mwaka mpya.
0 comments:
Post a Comment