December 02, 2024

WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA MUJIBU WA SHERIA

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Dkt. Zakia Mohamed Abubakar akizungumza wakati akifunga mafunzo ya kwa watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Disemba 01,2024.
 Na Mwandishi wetu, Arusha
Watendaji wa Uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga kura katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Dodoma wametakiwa kutumia elimu na ujuzi waliopata kwa ufanisi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria za uchaguzi.

Hayo yamesema Mkoani Arusha na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Dkt. Zakia Mohamed Abubakar wakati akifunga mafunzo ya kwa watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Disemba 01,2024.
 
Watendaji walioshiriki mafunzo hayo ya siku mbili ni Mratibu wa Uandikishaji wa Mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi, na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri kutoka mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na  kuwa ni vema wakatambua uzito wa jukumu lao katika zoezi hilo la kitaifa.
 
Dkt. Zakia amesisitiza umuhimu wa maafisa uboreshaji kuhakikisha kuwa wanasimamia na kuendesha zoezi la uboreshaji kwa umakini mkubwa.
 
Aidha, amewataka kusoma kwa makini na kuelewa maelekezo yote waliyopewa, kwani maelekezo hayo ni nyenzo muhimu za kufanikisha majukumu yao.
 
"Ni matarajio ya Tume kuwa, baada ya zoezi hili kukamilika, wale watakaopatiwa kadi watakuwa ni wapiga kura halali," amesisitiza Dkt Zakia.
 
Akifunga mafunzo kama hayo Mkoani Kilimanjaro, Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Balozi Omar Ramadhani Mapuri aliwahimiza watendaji wa uchaguzi mkoani Kilimanjaro kusimamia usambazaji wa mabango na vipeperushi mapema katika kata zote za halmashauri zao.
 
Balozi Mapuri pia amewataka maafisa hao kuhakikisha kuwa wanazingatia matumizi ya lugha nzuri na kuwapa kipaumbele wazee, walemavu, wajawazito, na kina mama wenye watoto wadogo katika vituo vya kuandikishia wapiga kura.
 
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoani Arusha, Mkoa wa Kilimanaro  na Mkoa wa Dodoma kwenye Halmashauri za Wilaya ya Kondoa, Chemba na Mji wa Kondoa kuanzia Disemba 11 hadi 17, 2024 ambapo vituo vitafunguliwa saa 02:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
Mwenyekiti wa mafunzo hayo akizungumza 

Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia hotuba ya kufunga mafunzo hayo. 
Meza kuu ikiwa katika mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani akizungumza jambo na washiriki wa mafunzo ya watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Disemba 01,2024.

Washiriki wa mafunzo kwa watendaji wa uboreshaji wa uboreshaji wa uchaguzi wakifanya mafunzo kwa vitendo. 
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Balozi Omar Radhani Mapuri akizungumza wakati akifunga mafunzo ya kwa watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Disemba 01,2024.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia hotuba ya kufunga mafunzo hayo. 
Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura w INEC, Bi. Giveness Aswile akizungumza jambno wakati wa mafunzo hayo Mkoani Kilimanjaro. 
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia hotuba ya kufunga mafunzo hayo. 
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia hotuba ya kufunga mafunzo hayo. 
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji Asina Omari akizungumza wakati akifunga mafunzo ya kwa watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambapo uboreshaji utafanyika kwenye Halmashauri za Wilaya ya Kondoa, Chemba na Mji wa Kondoa Disemba 01,2024.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia hotuba ya kufunga mafunzo hayo. 

No comments:

Post a Comment