December 07, 2024

MWANDUBWA ASISITIZA TAFITI KUIMARISHA UCHUMI

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Elijah Mwandumbya , akizungumza na hadhara wakati wa  Mahafali ya 38 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, duru ya pili, katika Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa, Kisesa Mwanza yaliyofanyika kwa mara ya 12 katika Kituo hicho.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Elijah Mwandumbya , akimkabidhi cheti cha pongezi Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo CPA. Dkt. Samwel Werema, kwa niaba ya Baraza la Uongozi wa Chuo kwa kusimamia vizuri miradi inayotelekezwa Chuoni hapo, wakati wa mahafali ya 38 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, duru ya pili Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa, Kisesa Mwanza yaliyofanyika kwa mara ya 12 katika Kituo hicho.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Elijah Mwandumbya, akimkabidhi cheti cha pongezi kwa kufanya vizuri katika masomo yake ya Shahada ya Mipango ya Maendeleo ya Mikoa, Bi. Rehema Leonard, wakati wa Mahafali ya 38 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, duru ya pili Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa, Kisesa Mwanza, yaliyofanyika kwa mara ya 12 katika Kituo hicho.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, akimtunuku mwanafunzi pekee aliyehitimu Shahada ya Uzamili ya Mipango Ufutiliaji na Tathmini Bw. Joseph Ochora, katika  Mahafali ya 38 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, duru ya pili Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa, Kisesa Mwanza, yaliyofanyika kwa mara ya 12 katika Kituo hicho.
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Wizara ya Fedha, Bw. Moses Dulle, akizungumza wakati wa Mahafali ya 38 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, duru ya pili katika Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa, Kisesa-Mwanza, yaliyofanyika kwa mara ya 12 katika Kituo hicho.
Baadhi ya wahitimu wakivaa kofia baada ya kutunukiwa shahada mbalimbali katika Mahafali ya 38 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, duru ya pili, katika Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa,  kilichoko Kisesa mkoani Mwanza, yaliyofanyika kwa mara ya 12 katika Kituo hicho.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (katikati), akiwa katika maandamano wakati wa Mahafali ya 38 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, duru ya pili katika Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa, kilichopo Kisesa mkoani Mwanza, yaliyofanyika kwa mara ya 12 katika Kituo hicho. Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Hozen Mayaya na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Maendeleo Vijijini CPA. Dkt. Samwel Werema.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahadhili wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, baada ya kuhitimisha kutunuku shahada mbalimbali kwa wahitimu katika Mahafali ya 38 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, duru ya pili, katika Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa, Kisesa Mwanza, yaliyofanyika kwa mara ya 12 Katika Kituo hicho.
*****************
Na. Josephine Majura na Saidina Msangi, WF, Mwanza
Serikali imetoa  rai kwa Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini  kufanya tafiti za bidhaa za mazao ya uvuvi, hususani kwa upande wa Ziwa Victoria ambalo kwa sehemu kubwa linagusa wananchi wengi wa Kanda ya Ziwa ili kuibua miradi ya kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi. 

Rai hiyo ilitolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Elijah Mwandumbya kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb,) kwenye sherehe za Mahafali ya 38 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, duru ya pili Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa, Kisesa mkoani Mwanza yanayofanyika kwa mara ya 12 katika Kituo hicho.

Alisema Serikali itaendelea kuwajengea uwezo wavuvi na wafugaji wa samaki ili waongeze uzalishaji, kuzalisha ajira, kuimarisha usalama wa chakula, kuongeza  kipato cha wavuvi na watu waliopo kwenye mnyororo wa thamani na hivyo kuchangia kwenye Pato la Taifa. 

‘‘Eneo linalopewa uzito wa hali ya juu na Serikali ni pamoja na elimu biashara, ufugaji wa nyuki, uvuvi, ufugaji wa mifugo, kilimo cha mazao ya nafaka pamoja na uongezaji wa thamani ya bidhaa ikiwemo bidhaa za uvuvi, kilimo, mifugo pamoja na  madini’’, alisema Bw. Mwandumbya.

Aidha, Bw. Mwandumbya aliuagiza Uongozi wa Chuo kuangazia sekta ya madini hasa ikizingatiwa kuwa ukuaji wa sekta hiyo umeongezeka na kuajiri vijana wengi ambapo kwa mujibu wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, inakadiriwa mchango wa sekta ya madini katika Pato la Taifa utaongezeka na kufikia asilimia 10 au zaidi kufikia Mwaka 2025. 

Alisisitiza kuwa eneo la madini ni eneo ambalo Chuo kinapaswa kuliangalia kwa jicho la aina yake na kushiriki kuchagiza uchumi wa Taifa kupitia tafiti endelevu na shirikishi za uongezaji wa thamani ya madini. 

Alilipongeza Baraza la Uongozi wa Chuo kwa kuendelea kukisimamia vyema Chuo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa ikiwemo fursa ya kuitumikia jamii kupitia miradi mbalimbali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo inayogusa watu wa chini katika jitihada za kuwainua kiuchumi, hususan katika sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji. 

Akizungumza na wahitimu Bw. Mwandumbya alisema kuwa ana imani kuwa ujuzi walioupata watautumia katika kuleta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali za maendeleo zinazoikabili jamii. 

Alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kuweka mazingira mazuri ya kujiajiri, hususan kwa kuboresha mazingira ya kufanya biashara na hivyo kuongeza fursa za vijana wakiwemo wasomi kujiajiri na hatimaye kupunguza tatizo la ajira.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya, alisema kuwa Chuo kimejizatiti katika kuandaa wataalamu wenye weledi wa kutosha katika fani za mipango ya maendeleo, kujenga moyo wa uzalendo na uadilifu kwa wataalamu hao ambazo ni nyenzo za msingi wa maendeleo  na ustawi wa nchi.

Aidha, alisisitiza kuwa Chuo kitaendelea kufuata kanuni zote za matumizi ya fedha ya umma ili thamani ya fedha ionekane. 

Naye Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo CPA. Dkt. Samwel Werema? alisema kuwa Chuo kinatarajia kuendela na ujenzi wa miundombinu katika Kampasi zote mbili za Dodoma na Mwanza ili kupunguza tatizo la mabweni kwa wanafunzi.

‘‘Chuo kitaendelea kuboresha mahusiano na wadau wa ndani na nje ili kuwa na ushirikiano thabiti na wa kudumu katika kazi za ushauri elekezi, mafunzo ya muda mrefu, muda mfupi na tafiti’’, alisema CPA. Dkt. Samwel Werema.

Aidha, alisisitiza kuwa Chuo kitaendelea kuhuisha mitaala ili kuendana na mahitaji ya soko pamoja na kuboresha shughuli za ushauri elekezi ili kutoa huduma bora inayokidhi mahitaji ya soko kwa wadau.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa Mwanza, Prof. Juvenal Nkonoki, alisema kuwa katika Mahafali hayo kulikuwa na jumla ya wahitimu 2,545 wanaume 1,156 na wanawake 1389 ikiwa ni ongezeko mara kumi ya idadi ya wahitimu wa Mahafali yaloiyofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 2011/12.

No comments:

Post a Comment