December 07, 2024

RAIS RUTO AMEFUNGUA MASHINDANO YA MICHEZO YA MABUNGE YA AFRIKA MASHARIK

Rais wa Kenya Mheshimiwa William Ruto akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika Mombasa Nchini Kenya 6-17 Desemba, 2024 huku Timu ya Bunge ikiwa inashiriki michezpo mbalimbali.
Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, Mheshimiwa Abbas Tarimba akizungumza katika ufunguzi wa Mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika Mombasa Nchini Kenya. Rais wa Kenya Mheshimiwa William Ruto amefungua rasmi mashindano hayo yalioanza tarehe 6 Desemba, 2024 na yanatarajiwa kumalizika Desemba 17, 2024.
Waheshimiwa Wabunge ambao ni wanamichezo wa timu mbalimbali za Bunge wakiwa katika hafla ya ufunguzi wa Mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika Mombasa Nchini Kenya. Rais wa Kenya Mheshimiwa William Ruto amefungua rasmi mashindano hayo yalioanza tarehe 6 Desemba, 2024 na yanatarajiwa kumalizika Desemba 17, 2024.


No comments:

Post a Comment