December 07, 2024

DKT. NCHEMBA ATETA NA UJUMBE KUTOKA BENKI YA DUNIA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao kati ya Serikali na Ujumbe wa Wataalam kutoka Benki ya Dunia, ukiongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete, kilichojadili vipaumbele vya miradi ya nchi itakayotekelezwa kupitia Dirisha Jipya la IDA21, kikao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade na Viongozi wengine waandamizi wa Serikali kutoka Wizara ya Fedha na Benki ya Dunia.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)




No comments:

Post a Comment