Shirika
la Reli Tanzania - TRC katika kipindi cha miezi minne tangu uzinduzi wa njia za
treni za umeme kati ya Dar es Salaam na Dodoma mnamo Juni 2024 limefanikiwa
kuingiza zaidi ya shilingi Bilinioni 20 baada ya kusafirisha abiria zaidi ya
1,000,000 (milioni moja).
Taarifa
iliyoyotolewa na Shirika hilo kupitia Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano, Fredy
Mwanjala zliyoitoz kwa umma imebainibisha
kuwa TRC inajivunia mafanikio hayo iliyoyapata katika kipindi kifupi cha kutoa
huduma kwa treni ya umeme ya mnwendo kasi maarufu SGR.
Mwanjala
amesema idadi hiyo ya abiria ni mara mbili ya abiria waliosafirishwa kwa mwaka
mzima na treni ya zamani.
“Idadi
hiyo ni mara mbili ya abiria waliosafirishwa na treni ya zamani (MGR), ambayo
ilisafirisha jumla ya abiria 400,000 katika kipindi cha mwaka mmoja. TRC
inatambua umuhimu wa huduma hii ya kisasa katika kuboresha usafiri, kuongeza
ufanisi wa biashara, na kutoa chaguo la haraka na salama kwa abiria, alisema
Mwanjala katika taarifa yake.
Aliongeza
kuwa “Tunafurahi na tunawashukuru abiria wetu kwa kuunga mkono jitihada zetu za
kuboresha usafiri wa treni za mwendokasi zinazotumia nishati ya umeme”.
Alisema
katika kipindi hiki ambacho TRC inashertehekea mafanikio, shirika lina
wahakikishia wateja na umma kwa ujumla kuwa litaendelea kutoa huduma bora zaidi
kwa abiria wake.
Aidha,
TRC inapanga kuongeza huduma zake na kuboresha miundombinu ili kukidhi mahitaji
ya wateja.
“TRC
inawaomba Watanzania kuipenda na kulinda miundombinu ya SGR ili iweze kuendelea
kutoa huduma yenye tija,”ilisema taarifa hiyo.
Treni za SGR kwa sasa zinafanya safari nne kutoka Dar kwenda Dodoma na zingine nne kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam kila siku ambavyo hutumia vituo vya Dar es Salaam, Pugu, Soga, Ruvu, Ngerengere, Morogoro,
Mkata, Kilosa, Kidete, Gulwe, Igandu na Dodoma kwa kupakia na kushusha abiria kulingana na aina ya treni.
No comments:
Post a Comment