Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete amekutana na kuzungumza Balozi wa Japan nchini Tanzania ambaye pia ni Mwakilishi wa Japan katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Yusushi Misawa pamoja na ujumbe wake alipomtembelea leo Novemba 18, 2024 katika Ofisi ya NSSF, Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo menbgine wawili hao wamejadili mambo mbalimbali ikiwemo kuwezesha vijana wa kitanzania nafasi za kujifunza kazi na kuimarisha mafunzo kuongeza ujuzi.
No comments:
Post a Comment