Nafasi Ya Matangazo

November 20, 2024

Shirika la Reli Tanzania - TRC katika kipindi cha miezi minne tangu uzinduzi wa njia za treni za umeme kati ya Dar es Salaam na Dodoma mnamo Juni 2024 limefanikiwa kuingiza zaidi ya shilingi Bilinioni 20 baada ya kusafirisha abiria zaidi ya 1,000,000 (milioni moja).
 
Taarifa iliyoyotolewa na Shirika hilo kupitia Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano, Fredy Mwanjala zliyoitoz kwa umma imebainibisha kuwa TRC inajivunia mafanikio hayo iliyoyapata katika kipindi kifupi cha kutoa huduma kwa treni ya umeme ya mnwendo kasi maarufu SGR.
 
Mwanjala amesema idadi hiyo ya abiria ni mara mbili ya abiria waliosafirishwa kwa mwaka mzima na treni ya zamani.
 
“Idadi hiyo ni mara mbili ya abiria waliosafirishwa na treni ya zamani (MGR), ambayo ilisafirisha jumla ya abiria 400,000 katika kipindi cha mwaka mmoja. TRC inatambua umuhimu wa huduma hii ya kisasa katika kuboresha usafiri, kuongeza ufanisi wa biashara, na kutoa chaguo la haraka na salama kwa abiria, alisema Mwanjala katika taarifa yake.
 
Aliongeza kuwa “Tunafurahi na tunawashukuru abiria wetu kwa kuunga mkono jitihada zetu za kuboresha usafiri wa treni za mwendokasi zinazotumia nishati ya umeme”.
 
Alisema katika kipindi hiki ambacho TRC inashertehekea mafanikio, shirika lina wahakikishia wateja na umma kwa ujumla kuwa litaendelea kutoa huduma bora zaidi kwa abiria wake.
 
Aidha, TRC inapanga kuongeza huduma zake na kuboresha miundombinu ili kukidhi mahitaji ya wateja.
 
“TRC inawaomba Watanzania kuipenda na kulinda miundombinu ya SGR ili iweze kuendelea kutoa huduma yenye tija,”ilisema taarifa hiyo.

Treni za SGR kwa sasa zinafanya safari nne kutoka Dar kwenda Dodoma na zingine nne kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam  kila siku ambavyo hutumia vituo vya Dar es Salaam, Pugu, Soga, Ruvu, Ngerengere, Morogoro, Mkata, Kilosa, Kidete, Gulwe, Igandu na Dodoma kwa kupakia na kushusha abiria kulingana na aina ya treni. 

Posted by MROKI On Wednesday, November 20, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo