Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amefanya mazungumzo kwa njia ya mtandao na ujumbe kutoka Idara ya Uvuvi na Wanyamapori ya Serikali ya Marekani kujadili pendekezo la Taasisi Zisizokuwa za Kiserikali la kupinga kuingizwa Marekani nyara zinazotokana na uwindaji wa tembo katika vitalu vya uwindaji wa kitalii kwenye eneo la West Kilimanjaro linalopakana na Hifadhi ya Amboseli Nchini Kenya.
Kikao hicho kimefanyika katika Makao Makuu ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) jijini Arusha leo Novemba 14,2024.
Ujumbe wa Marekani umeeleza kuwa vikundi vilivyopeleka pendekezo (petition) vinadai kuwa Tanzania inawinda tembo wa amboseli ambao wanafanyiwa utafiti, uwindaji huo unakiuka makubaliano ya miaka 30 ya kusitisha uwindaji katika eneo la West kilimanyaro - Amboseli, na unatishia kupotea kwa tembo wenye meno makubwa.
Waziri kwa kushirikiana na jopo la wataalam wakiongozwa wa Dkt. Alexander Lobora ametoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa uwindaji wa tembo, mchango wake katika uhifadhi na maendeleo ya jamii na kwamba uwindaji unafanyika kisheria kwa kuzingatia utafiti na uzoefu wa muda mrefu.
Aidha, Wizara imekanusha tuhuma hizo na imeushauri uongozi wa US Fish & Wildlife Service kupuuzia pendekezo lililowasilshwa na vikundi hivyo.
No comments:
Post a Comment