Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana(Mb) amekagua maabara ya ithibati (Acreditation)ya mazao ya nyuki inayosimamiwa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kupitia kituo chake cha utafiti wa Wanyamapori Njiro ambacho kimejikita kwenye utafiti wa nyuki na mazao yake.
Akikagua Maabara hiyo ya kuchakata mazao ya nyuki kwa viwango vya kimataifa leo Novemba 14,2024. Mhe. Chana ametoa wito kukamilisha maabara hiyo ambayo itaongeza pato la taifa kwa nchi kupata fedha za kigeni kupitia soko la kimataifa la mazao ya nyuki ikiwemo asali pamoja na uchumi wa moja kwa moja kwa wananchi.
“Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi Shupavu wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inahakikisha wananchi wananufaika na fursa zilizopo kwenye maliasili ikiwemo sekta ya nyuki“ amesema Mhe.Chana.
Naye, Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Wanyamapori Njiro, Dkt. Alfred Mariale amesema maabara ya ithibati itakamilika mwanzoni mwa mwaka 2025 na itasaidia kuharakisha biashara ya mazao ya nyuki katika soko la Kimataifa ambapo awali Serikali ilikuwa inatumia gharama kubwa kupeleka sampuli nje ya nchi kuthibitisha viwango vya ubora “Sample zilikuwa zinachukua miezi 6 kupata majibu na kusababisha kupoteza soko kupotea” ameeleza Dkt.Marriale
No comments:
Post a Comment