October 07, 2024

WAZIRI NDEJEMBI ARIDHISHWA NA KAZI NZURI MIRADI YA MAENDELEO SHINYANGA

Na Mwandishi Wetu, Kahama

Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi ameridhishwa na kazi nzuri ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa mkoa wa Shinyanga hatua hiyo inayompa faraja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Waziri Ndejembi amesema hayo Oktoba 7, 2024 katika ziara maalum ya kimkakati  ya akiwa halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wakati akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa vinne vinavyojengwa katika shule ya sekondari Mapamba.

Fedha iliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa madara hayo ni shilingi milioni 116.5 kwa ambapo Shilingi 104 ni kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na Shilingi 12.5 ni kwa ajili ya ukamilishaji wa chumba kimoja cha darasa. 

Hadi sasa fedha zilizotumika katika ujenzi wa madara manne ni Shilingi milionin 98.85 na imebadi Shilingi 17.6 na ujenzi huo upo katika hatua za kukamilisha samani zitakazotumiwa na wanafunzi.

Waziri Ndejembi  amesema suala la kubakiza fedha katika ujenzi  wa  Miradi ndiyo lakujivunia ambalo Rais Samia Suluhu analipokea sababu amekuwa akitafuta fedha za kuwanufaisha wananchi.

Akiwasilisha taarifa ya shule ya Sekondari Mapamba Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Rahel Wilson Mkuu wa amesema  ujenzi huo ulianza mwezi Julai, 2024 nakukamilika mwezi Oktoba mwaka 2024.

"Kukamilika kwa madarasa haya yatasidia kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa, kuongeza udahili wa wanafunzi wa kidato cha kwanza, kuchochea ufaulu wa wanafunzi kwa kuwa na mazingira rafiki ya kujifunzia, wananchi kuwa na imani na Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutekeleza maendeleo ya nchi kwa ukamilifu" amesema  Mwl. Rahel.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Annamringi Macha amesema madarasa hayo ni mazuri yanavutia wanafunzi kujifunza kwa kuwa miundombinu yake ni mizuri haijalishi iko vijijini au mjini.







No comments:

Post a Comment