October 07, 2024

KITUO CHA AFYA CHA SEGESE KUTOA HUDUMA NDANI YA MWEZI MMOJA

Serikali inatekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini ili kusogeza huduma karibu na wananchi badala ya kuzifuata huduma hizo umbali mrefu ikiwemo huduma za kiafya. 
 
Akikagua ujenzi wa Kituo cha Afya Segese kilichopo katika Halmashauri ya Msalala Mkoa wa Shinyanga, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi amwagiza Mganga Mkuu wa Hamashauri hiyo kuhakikisha Kituo hicho kinaanza kutoa huduma kwa wananchi ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa kwa kuwa baadhi ya majengo yamekamilika tayari kwa kutoa huduma. 
 
“Natoa mwezi mmoja Kituo cha Afya Segese kianze kufanya kazi mara moja baada ya kukamilika na kuwa na baadhi ya vifaa, uanze kwa kutoa huduma kwa wananchi hata vipimo vya awali” amesema Waziri Ndejembi.
 
Lengo la ziara ya kikazi ya Waziri Ndejembi ni kukagua miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Shinyanga inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  katika mkoa huo iendane na thamani ya fedha za Serikali ili kutoa huduma iliyokusudiwa kwa wananchi.
 
Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Msalala Dkt. Sisti Mosha kituo hicho 
kukamilika tangu mwaka jana na ila hakijaanza kutoa huduma kwa wananchi kwa kukosa nishati ya umeme, maji pamoja na watoa huduma wakiwemo Waauguzi.
 
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Msalala Dkt. Sisti Mosha amesema kituo hicho kimejengwa kwa gharama ya Sh. milioni 470 na kinatarajiwa kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje 12,000 kwa mwezi, wajawazito 1,260 na upasuaji 600 na hivi karibuni wanatarajia kupata madawa inatarajiwa kuwahudumia watu 36,247.
 
Hadi sasa baadhi ya majengo yaliyokamilika ni jengo la wagonjwa wa nje (OPD), maabara, eneo la upasuaji wakati Jengo la Mama na Mtoto halijakamilika kwa kukosa watumishi watakao toa huduma kwa wagonjwa, umeme pamoja na maji.



No comments:

Post a Comment