Nafasi Ya Matangazo

October 26, 2024




Na Happiness Shayo - Iringa 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amefanya ziara ya kushtukiza katika mradi wa ujenzi wa kituo cha utalii cha Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na kituo cha utafiti cha Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) inayotekelezwa chini ya mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW), Kihesa Kilolo Mkoani Iringa.

Mhe. Chana amejionea maendeleo ya mradi huo ambapo mradi wa ujenzi wa kituo cha utalii wenye thamani ya shilingi bilioni 21.4 umefikia asilimia 31 na kituo cha utafiti chenye thamani ya shilingi bilioni 1.55 kimefikia asilimia 80.

Ikumbukwe kuwa mnamo Septemba 7, 2024 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ilifanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi hiyo na kuelekeza Wakandarasi kusimamia mikataba yao na kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.

Mhe. Chana yuko Mkoani Iringa kwa ziara ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali iliyo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
Posted by MROKI On Saturday, October 26, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo