Na Mwandishi wetu, Morogoro
Watumishi wa Umma wanaoshiriki kwenye michezo ya 38 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), leo Oktoba 04, 2024 wamefanya matendo ya huruma kwa kurudisha kwa jamii kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Tshs Milioni 11.7 kwenye vituo vya wahitaji vya Manispaa ya Morogoro.
Mratibu wa zoezi hilo kutoka SHIMIWI, Itika Mwankenja amesema fedha hizo zimetoka mifukoni mwa washiriki takribani 3000 na wamenunua vyakula, madaftari, kalamu, maziwa ya watoto wa kuanzia siku moja, sukari, chumvi, sabuni, nepi za watoto pipi, juisi, viatu aina ya yeboyebo, na mafuta ya kujipaka, na wamepeleka misaada hiyo kwenye vituo vya Dalulu Muslim, Amani, Locaritch, Mgolole na Mission to the Homeless.
“Haya mahitaji muhimu tumegawa kulingana na uwingi wa watoto kwenye vituo hivi, maana vipo vyenye watoto 15 na vingine vina zaidi ya 40, pia tumepeleka na fedha taslim kuanzia laki 00 hadi nne ambazo watatumia kwa ajili ya kulipia huduma nyingine za umeme na maji, navyo tumevipa kulingana na idadi yao,” amesema.
Ametoa wito kwa jamii kuiunga serikali mkono katika kuvisaidia vituo vya wahitaji , ambavyo kutokana na uendeshaji wao unahitaji msaada mkubwa kutoka kwa jamii pamoja na serikali.
Naye Mlevi wa kituo cha watoto cha Mgolole, Sr. Mary Anitha ameshukuru watumishi wa umma kwa majitoleo yao kwa wahitaji, na amewaombea kwa Mwenyezi Mungu awasaidie katika kazi zao.
Sr. Anitha amesema kituo chao chenye kupata watoto kutoka Ustawi wa jamii baada ya kupatikana kwa taarifa za kina za mama wa mtoto husika, endapo anachangamoto za akili au amefariki na baba hawezi kumlea mwenyewe na hadi sasa kina watoto 56 wa kuanzia umri wa siku moja hadi miaka mitatu.
Mtoto Ritha Steven amewashukuru washiriki kwa zawadi walizowapelekea na kuwaomba waendelee kuwatembelea Mwenyezimungu awabariki.
0 comments:
Post a Comment