Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga leo Oktoba 12, 2024 ameungana na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na wananchi kwenye mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Jijini Mwanza.
Rais Samia yupo mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi ikiwepo kilele cha Wiki ya Vijana na Uzimaji mwenge wa Uhuru Kitaifa unaokwenda sambamba na Kumbukumbu ya miaka 25 tangu kufariki kwa Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
0 comments:
Post a Comment