Nafasi Ya Matangazo

September 27, 2024





Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi, Dkt. Pindi Chana amesema Serikali imejidhatiti katika utatuzi wa changamoto ya migongano kati ya wanyamapori na binadamu chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Ameyasema hayo leo Septemba 27, 2024  katika Semina ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Songea, Mkoani Ruvuma. 

"Mojawapo ya mikakati ya Serikali katika kutatua changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu nimetoa kibali kwa baadhi ya maeneo yenye changamoto tutavuna mamba, viboko na tembo kupitia uwindaji wa kitalii" amesisitiza Mhe. Chana. 

Aidha, amesema Serikali inatumia ndege nyuki (drones) kufukuza tembo, kujenga vituo vya askari uhifadhi na kufunga tembo viongozi kola kuzuia wasiingilie katika makazi ya watu.

Semina hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda, imehudhuriwa  na  Viongozi mbalimbali wa  Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) nchini.
Posted by MROKI On Friday, September 27, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo